HabariNews

Meli ya Maktaba MV Lagos Hope yaleta elimu Kenya

Meli ya maktaba tamba kubwa Zaidi ulimwenguni  MV Logos Hope iliwasili katika bandari ya Mombasa mapema Jumanne, Agosti 22.

Meli hiyo maarufu kama floating Library ilitia nanga saa tatu na nusu asubuhi ikimiliki vitabu zaidi ya 5,000 vyenye mada tofauti tofauti.

MV Lagos yenye urefu wa mita 132.5 iliwasili na watalii 350 kutoka mataifa mbali mbali ya kigeni.

Kwa siku 45 wakaazi wa Mombasa na maeneo tofauti nchini wataruhusiwa kuzuru meli hio na kujionea vitabu pamoja na mgahawa wa kimataifa.

Meli hiyo iliyopeperusha bendera ya Malta itafungua milango yake Jumatano hii Agosti 23 ambapo mkewe rais mama Racheal Ruto ataongoza hafla hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (KPA), Kapteni William Ruto aidha, amepongeza ujio wa meli hiyo, akiitaja kama ishara ya taifa kurudisha nafasi yake ya utalii wa meli ndani ya bahari hindi.

                               “Kama mamlaka ya bandari, tumepiga hatua kubwa kuboresha  mapokezi ya wageni, hasa kukamilika kwa kituo cha kisasa cha usafiri wa baharini, kuboresha viwango vya usalama kwa kufuata kanuni za kimataifa za Usalama wa Meli na Bandari (ISPS)”  Alisema .

BY EDITORIAL DESK