Ni kupoteza tu muda hakuna lolote la kumhusu mwananchi wa kawaida katika mazungumzo hayo.
Hii kauli yake naibu wa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua akipuzilia mbali mazungumzo ya maridhianao yanayoendelea kati ya Serikali na Upinzani.
Akizungumza katika kaunti ya Machakos Gachagua amesema hakuna matumaini yoyote kwenye mazungumzo hayo yatakayomwangazia mwananchi wa kawaida.
Gachagua amekariri kuwa Azimio haina nia ya kusuluhisha masuala ya yanayomhusu Mkenya wa kawaidia bali wanapigania uongozi.
“Hii mazungumzo ametuma Kalonzo pale, kwa ajenda hakuna maji ya Ukambani, hakuna mbolea, hakuna barabara, kwahiyo mazungumzo nini iko hapo? Mambo ya sava ni yenu? Kalonzo anazungumza nini kwa niaba yenu? amepatiwa ajenda na Raila na Ruto hakuweko.” Alisema Gachagua
Wakati huo huo Gachagua amewataka viongozi mbali mbali kuweka tofauti zao kando na kushirikina na Rais Ruto kwa minajili ya kustawisha taifa na kutatua shida zinazomkumba mwananchi wa kawaida.
“Raila alienda handshake na Uhuru Kenyatta hakumwambia Kalonzo, hakuenda na yeye, wakaenda kutengeneza makubaliano yake na Uhuru Kenyatta wakamalizana.” Alisema Naibu Rais.
“Project zote alitoa kwa Uhuru akapeleka kwao, kuna project alileta hapa ukambani? Lakini nyinyi hata hatuelewi nyinyi. Sasa ametafuta rais juzi hakuja na Kalonzo.” Aliongeza Gachagua.