HabariMombasaNews

INASIKITISHA, Barayan apaza Kilio cha wenye mahitaji Maalumu

Fatma Bakari Barayan awataka viongozi kutoka ukanda wa pwani kubuni sera zitakazo nufaisha jamii za wapwani hasa wanaoishi na mahitaji maalumu.

Barayan ambaye ni Mwenyekiti wa hazina ya fedha ya kibiashara ya vijana nchini, alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baadhi ya viongozi waliopewa nafasi ya kuongoza wameeka nyuma maslahi ya wananchi.

“Mimi naomba kwanza viongozi wa Mombasa muchukue jukumu, Uongozi nikama amana nakuangali sekta mbali mbali ikiwemo wenzetu wanao hitaji mahitaji maalum. Tuungane pamoja na kuweka mikakati ambayo tutaweza kuwawezesha kiuchumi na kupata zile huduma na nafasi ambazo ziko katika seerikali” Alisema.

Barayan alizungumza haya katika hafla ya kuwezesha jamii zinazoishi na mahitaji maalumu kaunti ya Mombasa, iliyoandaliwa na naibu mwenyekti wa chama cha UDA Hassan Sarai.

Hali kadhalika Kiongozi huyo alighadhabishwa na hatua ya baadhi ya viongozi kutumia jamii hizo kisiasa badala ya kuwainua kimaisha.

“haki zao hawapewi sababu kuna ule mgao kutoka kule serikali kupitia kaunti iliwawezekupewa ule mgao wajiendeleze kiuchumi na vile vile masuala ya maisha yao, lakini wengi wao wanaweza shuhudia leo hii, hata ule mgao pia hawapati” Aliongezea Barayan.

Swala la ukosefu wa ajira halikusazwa, kiongozi huyo aliwasihii wakaazi wa pwani kukumbatia shughuli za kibiashara huku serikali ikiweka mikakati ya kuwaajiri katika taasisi mbali mbali.

“Itachukua muda labda miezi miwili, mitatu ama minne, lakini hizi nafasi za kazi zitakuja na tutaweza kuwasindikiza muajiriwe pale bandari, muajiriw youth fund, muajiriwe NACADA na muajiriwe kwenye hizi taasisi na halmashauri zingine, ili muweze kusaidia jamii kwa jumla”       Alimalizia na amewataka kuwa na subira kwani muda mwafaka unawadia.

BY DAVID OTIENO