Imebainika kuwa zaidi ya wakazi elfu 10 kaunti ya Kilifi wanaugua maradhi ya kifafa.
Katibu wa Kamati ya Kitaifa inayoshughulikia maswala ya ugonjwa wa Kifafa, Fredrick Beuchi, alithibitisha haya akisema kuwa kaunti ya Kilifi ipo na visababishi vingi vinavyochangia ongezeko la ugonjwa huo.
Hatua imepelekea kaunti hiyo kuorodheshwa miongoni mwa kaunti zilizo na idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa huo hapa nchini.
“Kuna sehemu ambazo zimeonekana kuathirika pakubwa kutokana na vyanzo vinvyo changia ugonjwa huu, moja ya sehemu hizi ni kilifi kaunti. Kwa sasa watu Zaidi ya elfu kumi wako na hali hii ya kifafa kaunti,” alisema Fredrick
Hili linajiri huku kukiwa na hofu kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka Zaidi katika sehemu hio kufuatia hatua wataalamu kuendelea kufanya tafiti zao pasi na kutoa suluhu mwafaka ya maradhi hayo.
“Takwimu hizi ni za muda kwa hivyo kuna uwezekano ya kwamba kukifanywa tafiti zengine zozote zile basi watu wamezidi na juhudi za kufanya tafiti zinaendelea.” Aliongewea.
Kulingana na takwimu, watu zaidi ya milioni 1.5 wanaugua aina mojawapo ya hali hii ya kifafa hapa nchini.
BY EDITORIAL DESK