HabariNews

Kwa Pamoja Twaweza! Mashirika ya Kijamii yaungana Pwani

Baadhi ya Mashirika ya kijamii yameungana chini ya Mwavuli wa Jumuiya ya Mashirika ya Pwani kama njia moja ya kuweza kuunganisha mashirika hayo ukanda wa Pwani

Yusuf Lule kutoka shirika la HuRIA mojawapo ya mashirika Mombasa ,Pwani alisema kuwa hatua hiyo itaweza kuleta umoja wa Wapwani kupitia mashirika hayo.

Lule alitaja kuwa umoja wa mashirika hayo utakuwa chombo cha kupeleka agenda za maendeleo kiuchumi na siasa ukanda huo.

“Uzinduzi huu ni muhimu sana kwetu sisi kama mashirika kw sababu ni chombo ambacho kitatusidia sisi kama asasi zisizokuwa za kiserikali kupeleka agenda za maendeleo kwa miaka mingi tumekuwa na vyombo tafauti tofauti ikiwemo wanasiasa amabao wametuzwa majukumu ya kuhakikisha kwamba yanasukuma maendeleo lakini wanafanaya kazi kati hali tofauti tofauti tumeina ipo haja ya kuanzisha vuguvugu kama hili.” Alisema Lule

Kwa upande wake Evans Kasena Mkurugenzi kutoka shirika la Haki Aafrika, muungano huo utawezesha jamii kujumishwa serikalini ikiwemo kushughulikia mambo ya afya na kuwezeshwa kwa jamii zilizoko eneo la Pwani, akitolea mfano wanawake na vijana kuhusishwa katika mambo ya maendeleo na kuwa kioo kwa viongozi waliochaguliwa eneo hilo.

“Tuko na mambo taofauti tofauti kama vile uongozi, jamii kujumuishwa katika mambo ya srikali ya kaunti, pia maswala ya afya mimba za mapema na mengineyo.” Alisema Kasena.

Muungano huo unanuwia kuwaleta pamoja vijana wote Pwani kuchukua nafasi za uongozi katika mashirika

BY EDITORIAL DESK