HabariNewsTravel

NAULI MOTO; Shule zafunguliwa Rasmi, Wanafunzi wakitatizika Kiusafiri

Shule zimerejelea masomo kote nchini katika muhula wa tatu Agosti 28,2023. Furaha hii ya wanafunzi iliandamana na kilio cha Wazazi kulalamikia gharama ya juu ya nauli wanaodai kufikia sasa ni ghali mno.

Sekta ya uchukuzi iliooteshwa vidole vya lawama mjini Mombasa, ilipandisha nauli maraduru kado na matarajio. Safari ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi ikigharimu shilingi 2500 kutoka 1500 ksh. Anayeelekea Kisumu akiongezewa nauli kutoka Ksh. 2500 hadi Ksh. 3500

“Rush inakuwa upande mmoja sio upande zote mbili ndo maanake tunaeka fare kuwa juu kwa sababu tukifika kule mahali tunakwenda huwa atakuna hata mtu wa kurudi nae.’’Alisema Abdulhakim Abud

Hata hivyo madereva wamejitetea kuwa hali hii imechangiwa na gharama ya juu ya bei ya mafuta pamoja na hali ya wanafunzi wengi kutoka ukanda wa pwani kusomea sehemu zingine za nchi.

“Kama ni back to school utapata watoto wengi wanasomea bara akuna watoto wa bara kuja kusomea pwani. Wengi wao huwa wanatoka pwani wanaenda kusomea bara. Na sasa ukitoka hapa pwani ukienda bara wakati wa kurudi hivi abiria hana.Sasa wakati wa rush inakuwa wakati wa kurudi ni hasara unatafuta tu pesa ya mafuta unarudi.’’ Alisema Salim Mzee wa Busara.

Kulingana  na uchunguzi wa meza yetu ya habari, gharama ya nauli imepanda kwa zaidi ya asilimia 50 hatua inayopelekea baadhi ya wanafunzi kukwama katika vituo vya basi kwa sababu ya ongezeko hilo.