HabariNews

Masomo Yakatizwa, Smart Start Academy Ikifungwa  Kongowea

Shughuli za masomo zilitatizwa katika shule ya kibinafsi ya Smart Start Academy, Kongowea eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa baada ya maafisa wa utawala kufunga shule hio mapema Agosti 29, 2023.

Kwenye taarifa na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu  wa shule hiyo Kelvin Ondiek alikashifu vikali hatua hiyo akiwalaumu maafisa hao waliodai kuwa shule hiyo haijasajiliwa na haikuwa na vigezo hitajika vya miundo msingi .

Madai hayo yalikanushwa vikali na Ondiek aliyesistiza kuwa idara ya afya ya umma na ile ya elimu ilifanya ukaguzi katika shule hiyo huku akiwalaumu machifu kwa kuingiza siasa katika swala la elimu.

Watu wa afya walikuja wakafanya ukaguzi wao, ni shughuli inayoendelea lakini nashangaa wameingiza siasa kiasi cha kwamba wanataka kuangamiza maisha ya watoto wetu.”alisema Ondiek.

Kwa upande wao wazazi walishikilia kuwa hawataruhusu wanao kuhangaishwa na kuitaka serikal kuingilia kati na  kusuhisha mzozo huo.

Machifu wasiokuwa na nidhamu wakachukua mwelekeo wa kuja kutusumbua kutoa watoto darasani sasa kitu ninachoomba mimi, naomba serikali ifatilize hili jambo.” Alisema Famau

Hili linajiri tu baada ya shule kufunguliwa rasmi kwa muhula watatu Agosti 28, 2023.