Jamii ya Dzitengezere katika eneo bunge la Nyali kaskazini hatimaye imepata hatimiliki ya ardhi ya ekari 5.9 ambayo wamekuwa wakizozania mahakamani kwa muda mrefu.
Jamii hio ilipokea hatimiliki ya ardhi yao katika kanisa la KWA RASTAR kwa mbwembwe wakishabikia ushindi huo kwa kuhimiza ushirikiano kudumishwa miongoni mwao.
Akizungumza katika sherehe hio wakili aliyewakilisha jamii hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa mashirika yasiyo ya kiserikali ukanda wa pwani Zedekia Adika, aliitaka serikali ya kauti kuwafanyia sahali jamii hio na kuwaondolea deni la shilingi milioni 39 linalowakabili iliwaweze kuendeleza maisha yao.
“Katika hii percel kuna loan ya land rate ya 39 million, hawa watu wanapata hii title deed leo, hii pesa itolewe ndio hawa watu waanze maisha afresh. Tunaomba afisi ya msajili na sorovea wa Mombasa na serikali kuu kwamba hawa watu wasaidike ili waweze kupata title deed kwa majina yao.” Alisema
Adika alisema kuwa unyakuzi wa ardhi ukanda wa pwani umekuwa Donda sugu hali inayopelekea wamiliki halali wa ardhi kuishi kama maskwota.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jamii ya Dzitengezere Selestin Kachando amewataka wanajamii hao kusalia na umoja hata baada ya kupokea cheti hicho cha hatimiliki huku akimtaka gavana Abdulswamad kuingilia kati kati suala la deni linalowakabili.
“tunaloomba serikali ya kaunti mutuunge mkono maana kunayo hio deni ya rates 39 million iweze kuondolewa gavana wetu Abdulswamad unapopata sauti yetu na kilio chetu tusikie, iliyakwamba tuweze kuondoa hio rate,” Selestin alisema.
Jamii hiyo hatahivyo inadaiwa kuishi kama maskwota katika ardhi hiyo kwa kwa zaidi ya miaka 25. Kando na eneo hilo la kazandani, maeneo mengine yaliyo na migogoro ya mashamba ni pamoja na eneo la Moroto, Padia, Balala na maeneo mengine sehemu hiyo.