HabariKimataifaNewsWorld

Jamaa AMUUA Mwenzake kisa Ushabiki wa Mechi kati ya Arsenal na Man U, Uganda

Shabiki wa Klabu ya Kandanda Arsenal alidaiwa kudungwa kisu hadi kufa na shabiki wa Klabu ya Manchester katika eneo la sheema magharibi mwa Taifa la Uganda.

Kulingana na Asasi za kiusalama wakiongozwa na msemaji wa kitengo hicho Marcial Tumusiime, Jackson Aineruhanga mkaazi wa Rwanyinakahire, wadi ya Rwamujojo alidungwa kisu baada ya kutamatika kwa mchezo huo ulioishia 3; 1 ugani Emirates.

Tumusiime alisema kuwa ugomvi wao ulianza baada ya bao la mchezaji wa Man U Alejandro Garnacho kukataliwa na kupitia teknologia ya VAR.

“Inadaiwa jioni ya Septemba 3, 2023, palizuka ugomvi kati ya Aineruhanga na mshukiwa katika banda la video walipokuwa wakitazama mpira wa miguu kati ya Manchester na Arsenal. Wawili hao walielekea katika bar moja ambapo walikataliwa, hili lilimpelekea mshukiwa kumkimbilia na kumdunga kifuani kutumia ala ya kupata. Mwathiriwa anadaiwa kufaariki baada ya kupoteza damu nyingi kutokana na shambulio hilo.” Alithibitisha Tumusiime.

Hadi kufikia Jumanne jioni mshukiwa alikuwa bado mafichoni huku Tumusiime akisema kuwa kipande cha kijiti kilichoshukiwa kuwa na mabaki ya damu kilipatikana katika eneo la tukia na maafisa wa upelelezi.

“Mshukiwa alivaa viatu vya wazi ambavyo vilipatikana katika eneo la tukio. Mwili wa Aineruhanga umepelekwa katika kitua cha afya level IV kwa ajili ya upasuaji” Alisema.

BY EDITORIAL DESK