HabariNews

Ubaguzi wa Uteuzi Katika Kongamano la Kujadili Tabia nchi, Haki Afrika Yalia

Kongamano la Mabadiliko ya hali ya anga Barani Afrika lililoandaliwa jijini Nairobi limekosa kuwajumuisha kikamilifu waathiriwa wa mabadiliko ya Tabianchi na badala yake kuwathamini zaidi wale wanaochangia uharibifu wa hali ya hewa.

Haya ni kwa mujibu Naibu mkurunguzi wa shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini Salma Hemedi, kongamano hilo limeundwa kujumuisha wakilishi kutoka mashinani haswa kutoka maeneo ya ukame na wala sio kuangazia wafadhili kutoka mataifa ya kigeni

Tukiangalia hili kongamano tunaona utafauti wake ni kuwa wageni kutoka nchi mbali mbali wamekua kwa asilimia kuu zaidi ya wanati wa nchini, lakini sisi kama shirika la Haiki afrika tunaona kwamba kuna uwepo na haja kwamba bado hili kongamano lingeweza kuleta watu ambao wanaathirika kwa hali ya juu sana” Alisisitiza Salma

Salma alisema kuwa wakereketwa wengi haswa wale wa mazingira na watetezi wa haki za kibinadamu walizuiliwa kuhudhuria kongamano hilo ili wasiweze kusema dhulma zinazochangiwa na mataifa hayo tajiri.

letu ambalo limetuendekeza sisi kufanya maandamano ni kwa sababu ya kutohusishwa kwetu katika hili kongamano.Tulisajili kwa wakati hadi nilipokuwa naenda kuchukua kibalichangu hawakutujibu kwamba kuna wengine hawakupata hio stakabadhi isipokuwa nilipokwenda wanasema kwamba ile process haikuweza kupitishwa, na wanaangalia huyu anaongelea masuala gani, naelewawa ni kwanini pengine wangemnyima sababu wanajua atakapo Kwenda pale ataliongelea lile swala ambalo wao hawataki kuliongelea” aliongezea

Salma hata hivyo aliongeza kuwa ni lazima mataifa ya bara Afrika yaangazie maslahi ya wananchi wake na kuzuia dhulma haswa za uharibifu wa mazingira inazochangiwa na mataifa yaliyoendelea ulimwenguni.

 

BY EDITORIAL DESK