Partrik Mbelle, Mwakilishi wadi Ya Bamburi ambaye pia ni mweneykiti wa kamati ya uchumi samawati katika bunge la kaunti ya Mombasa aliwataka mabwenyenye wanaomezea mate vipande vya ardhi baharini kukoma la sivyo chuma chao kimotoni .
Akizungumza katika kipindi cha sauti asubuhi Mbelle, alisema kuwa ili kufanikisha maendeleo yanayoshinikizwa na mpango wa uchumi samawati kwa wavuvi kutoka pwani hasa Mombasa ni sharti wasimamizi wa fuo za bahari BMU wasajiliwe kama vyama vya ushirika.
Hatua hii kwa upande mwingine inapata pingamizi kutokana na ukosefu wa hati miliki.
Kulingana na Mwenyekiti huyo baadhi ya sehemu katika ufuo za Bahari zinapaswa kutumiwa na BMU ila mabwenyenye hao wamekita kambi na kuchangia kuzorotesha shughuli za uvuvi.
“Hawa wavuvi kidogo ndio wamepata peke yake na sababu ya kuwa wamepata ni kwamba wao ndio wako na title deeds peke yake, hizi BMU lazima wapewe title deeds ndio waweze kufaidi katika huo mradi, pesa hawapewi mpaka wawe nazo. Shida ni kwamba katika zile sehemu zao kuna watu wajanja wamenda pale kwenda kugrab zile places na mapema , as long as mimi ni chairman wa blue economy committee tutapambana” alisema .
Serikali kwa upande wake imeweka mikakati ya kutoa hamasa ya kutosha ili kufanikisha elimu hiyo licha ya wavuvi kuwa na changamoto za kutoelewa maswala ya vyama vya ushirika.
Mbelle hatahivyo alionyesha matumaini ya kuimarika kwa sekta ya uvuvi pwani utaimarika iwapo mfumo huo utakumbatiwa kikamilifu kwani ipo mipango ya kutoa mikopo kwa vyama hivyo vya wavuvi kununua bidha za kisasa za uvuvi.