HabariNews

PIGO! Mahakama ya Upeo Yadinda kusitisha Utekelezwaji wa Sheria tata ya fedha 2023

Mahakama ya Upeo imedinda kusitisha utekelezwaji wa sheria tata ya fedha ya mwaka 2023.

Katika uamuzi uliotolewa Ijumaa 8, 2023  mahakama hiyo ya Kilele imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na seneta wa Busia Okiya Omtatah na wengine waliotaka sheria hiyo kusitishwa.

Katika uamuzi huo mahakama iliamua kuwa haina mamlaka kuruhusu rufaa hiyo huku ikiongeza kuwa haijashawishika kuwa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ulikiuka haki katika kuthibitisha mamlaka yake.

Vile vile mahakama ilifutilia mbali rufaa zote zilizowasilishwa kwao ikisema kuwa hazikuwasilishwa kwa wakati ufaao.

Ikumbukwe kuwa awali Jaji wa Mahakama ya Juu Mugure Thande alikuwa ametoa maagizo yaliyosimamisha Sheria hiyo ya Fedha hadi kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah.

Mnamo Julai 2023, Mahakama ya Rufaa iliondoa amri ya kuzuia utekelezaji wa sheria hiyo, ambayo pamoja na mambo mengine iliongeza maradufu Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za mafuta ya petroli hadi asilimia 16 na kuanzisha tozo ya nyumba ya asilimia 1.5.

BY MJOMBA RASHID