Mwanaharakati wa kushughulikia watu wenye matatizo ya akili kaunti ya Mombasa Amina Abdalla ameeleza haja ya kuundwa kwa sheria bungeni kuwalinda watu hao katika jamii.
Akizungumza na meza yetu ya habari Amina ambaye ni Mwenyekiti na Mwanzilishi wa shirika la Mombasa women Empowerment alitilia mkazo suala la matatizo ya kiakili akisema hupelekea watu wengi kujipata barabarani wakiranda bila mwelekeo na linafaa kushughulikiwa kwa dharura serikali.
Vile vile kiongozi huyu aliwataka vinara katika bunge la kitaifa kushirikiana na kuhakisha sheria inabuniwa kukabiliana kikamilifu na ongezeko la watu wanaorandaranda kutokana na matatizo ya kiakili.
“Tushirikiane ili hawa wagonjwa tuweze kuweka sheria bungeni, na kuweza kuwastiri ndugu zetu vile vile watu wa UKIMWI wanavyosaidika vile vile watu wa TB wanavyosaidika basi waathiriwa wa akili pia ni haki yao kuweza kusaidiwa , na hakuna kitu ambacho ni kibaya katika serikali na wananchi kama kuweza kuugua a. Kama kuna kitu ambacho serikali inafaa kutilia maanani ni mtu ambaye akili zake haziko salama.” Alisema Amina.
Wakazazi aidha katika kaunti ya Mombasa walisikitishwa na hali hii wakipendekeza serikali kuwa na mpango wa kuwatafuta wote wanaokumbwa na matatizo hayo ili kuwahifadhi katika makaazi maalum pamoja na kujenga vituo vya kuwasaidia.
“Mimi ningependa serikali ije na mipango ya kubuni mahali kama rehabilitation,” Alipendekeza mmoja.