Wakulima wa maembe eneo la dzombo katika kaunti ya Kwale wameanzisha mtambo wazao hilo unaolenga kuongeza thamani kwa maembe na kupunguza hasara ya mazao baada ya kuvuna.
Hazina ya utafiti nchini NRF na taasisi ya KALRO ilijiunga na wakulia kufadhili ujenzi wa kiwanda hichi cha maembe kilichogharimu takriban shilingi 3m.
Wakulima hao wamekuwa wakikadiria hasara licha ya wingi wa zao hilo kutokana na madalali wanaonunua maembe kwa bei duni. Hasara hio imekuwa ikiwavunja moyo wakulima wengi katika eneo hilo.
“ kuna yale maembe tulikuwa tunafikiria hayafai saii tunaweza kuyasaaga kuwa juici na tunapata jam. Sahiii faida ni kwamba hakutakuwa na hasara kubwa,” alisema mmoja wa wakulima.
“wale wannunuzi wakinunua maembe huwa wanayachagua, wanachukua makubwa alafu madogo wanayaacha kuoza na ilikuwa inaumiza sana. Hatutafanya biashara kama kawaida, tutaunganisha wakulima na mashoko bora ili waweze kupata pesa zaidi ” aliongezea afisa wa KALRO – Finyange Pole
Kulingana na Masoud Chigona, mwenyekiti wa wakulima dzombo, ujenzi wa kiwanda hicho umewaletea afueni wakulima ambao walijiunga na chama cha ushirika cha wakulima ili kutafuta njia ya kukabili tatizo hilo.
“Kwa sasa kwa kweli ni kwamba hatutatupa kittu , kwasababu la kuvujika litaenda kwa solar drier, lile ambalo limeiva tutalisaga hapa yale megine tutauza, kwahio mkulima hapa amefaidika sana na atapata pesa kulingana na yale mazao amepanda” alisema Chigona.
Vile vile mwenyekiti wa NRF Ratemo Michieka, alisifia ujenzi wa kiwanda hicho akikitaja miongoni mwa miradi itakayomkuza mkulima mdogo na kuwezesha azma ya serikali ya kukuza wananchi wa tabaka la chini.
“itasaidia kwa hakika wakulima wadogo katika maeneo haya ya nchi kwale , na ninauhakika kazi kama hizi zitasaidia serikali kuhakikisha kua watu wa tabaka la chini wananufaika kutokana na mradi huu” alisema Ratemo
mkurugenzi mkuu KALRO Eluid Kireger aaidha alitoa wito wa ujenzi viwanda sawia na hiki kutokana na gharama ya chini ya ujenzi inayopelekea manufaa mengi kwa wakulima wadogo wadogo.
“ tunaamini kuwa hii ndi mkondo unaofaa kwa sababu kiwanda hiki si ghali na kinaweza kupatikana na wakulima wadogo na wito wetu ni kuwa mradi kama huu uweze kufanyika sehemu nyingine ili kukuza wakulima” alisema Kireger
Bidhaaaaaaa za mvinyo siagi sharubati pamoja na keki zikitengenezwa katika kiwandi hiki chenye takriban wafanyikazi 20 na kilicho na uwezo wa kusaga tani 4 za maembe kwa siku na kukausha tani 2 kwa wiki.