Mahakama ya Shanzu imetoa uamuzi wa kuendelea kuzuiliwa kwa mhubiri tata Paul Mackenzie na washukiwa wengine 28 kwa siku 30 zaidi.
Haya yamejiri baada ya Wakili wa Mackenzie Wyclife Makasembo kuwasilisha ombi la kutaka vikao vya kesi yake kuahirishwa kwa muda wa wiki mbili ili kumpa fursa ya kutibiwa.
Kwa mujibu wa Makasembo mteja wake alipuziliwa kemikali iliyomfanya kuhisi kisunzi na hatimaye kuibiwa vitu vyenye thamani.
Awali upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la kutaka Mackenzie na washukiwa wengine kuzuiliwa kwa miezi 6 ili kuupa upande huo muda wa kufanya uchunguzi dhidhi yao mahaka ikisema ombi hilo litajadiliwa baada ya siku hizo 30 kukamilika.
Kufikia sasa Mackenzie amezuliwa kwa zaidi ya miezi 5 bila kufunguliwa mashataka tangu alipokamatwa tarehe 15 Mwezi Aprili mwaka huu akikamilisha takribani siku 156 bila kushatakiwa.
Aidha Mackenzi na washukiwa wenza wanakabiliwa na makosa yasiyopungua 12 yakiwemo mauaji, ugaidi, kuwasaidia watu kujiua, uhalifu dhidhi ya binadamu, utekajinyara, itikadi kali, mauaji ya halaiki, ukatili dhidi ya watoto, ulaghai na utakatishaji wa fedha.