Kamati ya mazungumzo ya maridhiano imesema shughuli ya kupokea watu wanaotaka kushirikishwa kwenye mazungumzo ya upatanishi itendelea hadi Ijumaa hii tarehe 22.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti mwenza katika kamati ya kitaifa ya mazungumzo Kimani Ichung’wah wataanza kusikiliza mapendekezo ya watu hao kuanzia Ijumaa wiki hii huku kila upande ukipewa dakika 20 za kuwasilisha mapendekezo yake mbele ya kamati hiyo.
Kamati ya kiufundi ya tume ya uchaguzi IEBC, ile ya uwakilishi wa kijinsia na kamati ya uteuzi zitafika mbele ya kamati hiyo kuwasilisha mapendekezo yao.
”Tumekubaliana kwamba tutaanza kusikiliza maoni ya wananchi ijumaa wiki ijayo na kil upande utakuwa na dakika 20 kuwasilisha mapendekezo yake.” Alisema Ichung’wa
Kalonzo Musyoka anayewakilisha upande wa Azimio alisema wanachama wa kamati hiyo watakutana Alhamisi wiki hii kujadili maswala kadha wa kadha.
“Tutakuwa na kongamano la wazi siku ya ijumaa ambapo tutakuwa tunasikiliza maoni ya wananchi tunamatumaini kutapata chumba kikumbwa cha kufanya majadiliano katika ukumbi wa Bomas.” Alisema Musyoka.
Vikao vya kusikiliza mapendekezo ya Wakenya na makundi mbalimbali vitaendelea hadi wiki ijayo na baada ya hapo kamati ita tathimini maoni yote kabla ya kuandika ripoti ambayo itawasilishwa bungeni baada ya siku 60 kukamilika.