Vijana 500 kutoka kaunti ya Kilifi wamenufaika na ufadhli wa elimu kutoka shirika la Power Learn Project itakayowawezesha kupata mafunzo kupitia njia ya mtandao ili wajitafutie ajira na kujikimu kimaisha.
Kwa mujibu wa afisa mkuu wa mipangilio katika shirika hilo (Chief Growth and Operations) Mumbi Ndungu, mafunzo hayo yatawasaidia vijana kupata ujuzi wa kitekinologia ya kutengeneza mitandao ambayo itawasaidia kujiendeleza kimaisha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika chuo kikuu cha Pwani Ndungu, alisema kuwa vijana wote kutoka wadi 35 walinufaika na ufadhili huo unaotarajiwa kuchukua muda wa miezi 4.
“tumeweza uzindua hii program ambako tunapatia vijana 500 kutoka wodi mbali mbali huku kaunti Ya Kilifi ufadhili, wataweza kusoma kwa muda wa miezi minne tutawafundisha kuhusu digital skills ambapo baada yake wataweza kutumia ujuzi huo kutafuta riziki, wataweza kupata kazi huku au hata nje ya nchi ambacho sisi kama powerline husaidia nacho. Training yetu sana sana hufanyika online,”
Kwa upande wao baadhi ya vijana walionufaika na ufadhili huo Wakiongozwa na Mohamed Almasi na Rose Heri, walielezea matumaini yao wakisema kuwa wengi wao wamekosa ujuzi wa kujitafutia ajira kupitia njia za kidigitali .
“Vijana wengi wamejiunga kwa sababu kuna suala kubwa la ukosefu wa kazi na ktika digital economy kuna nafasi nyingi ni vile tu unapata vijana wengi hawana maarifa kama haya ndio maana unaona vijana wengi wamejiandikisha” “tuko na shida ya employment Kenya na imeathiri mayouth sana , so hii program vijanaa watapata ujuzi unahitajika waweze kujitafutia nafasi za ajira katika ulimwengu wa dijitali,” walisemaa baadhi yao.