Wanafunzi katika kaunti ya Mombasa wamehimizwa kukumbatia ubunifu wa michezo ya teknolojia ili kuwawesha kimasomo hususan katika mtaala mpya wa CBC.
Akizungumza katika kongamano la Tech Kidz Africa lililofanyika ndani ya ukumbi wa sanaa Swahili pot Valentine Kwamboka, ambaye ni mwalimu katika maswala ya teknolojia alisema mafunzo hayo yanalenga kuwaelimisha wanafuzni kisaikolijia na pia kuwaelimisha kuhusu ulimwengu wa mtandao.
Kwamboka aidha aliwataka wanafunzi kukumbatia elimu ya teknolojia badala ya kurandaranda mitaani na kujihusisha na utovu wa nidhamu huku wakishirikiana na washika dau mbali mbali ikiwemo Rasp berry p1,Close the Gap Kenya, Code Innovators, Compassion International na mengineyo nchini, kutoa masomo kwa wanafunzi.
“Somo hili linajumuisha mambo mbalimbali kama vile Robotic,Coding na Gamification ambapo husaidia mwanafunzi kutengeneza mchezo wake mwenyewe,pia hufanya mtoto kuwa na shughuli ya kufanya badala ya kujiingiza kwa mihadarati”. Alisema Valentine.
Festus Kiluli na Ruth Mnyasi walimu katika shule ya Upili ya Mbarak walisema kuwa masomo hayo yatawawezesha wanafunzi hao katika masomo ya kisanyansi kwa ujuzi wanaopata huku wakitoa wito kwa shirika hilo kupanua wigo wake kwa shule za chekechea ili kunufaisha wanafunzi wengi kuhusu teknolojia.
Walimu hao vile vile walitoa wito kwa wazazi kuwaelimisha na kuwahimiza watoto wao kukumbatia masomo ya teknolojia kutokana jisnsi walimwengu wanavyokumbalia mfumo wa dijitali.
“Mafunzo haya yatawezesha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi kama vile fizikia,kemia na bayologia kwani baadhi ya mambo ambayo wanasoma yanaendana na masomo haya,pia tunaomba serikali ya kaunti ishirikiane na shirika hili ili mafunzo haya yafikie shule nyingi kwa manufaa ya wanafunzi”,walisisitiza walimu.