Ajali Barabarani na uvunjaji wa kanuni zake huenda ikapungua pakubwa katika kaunti ya kilifi baada ya munispaa ya malindi kupokea alama za barabarani zinazotarajiwa kutoa suluhu kwa changamoto zinazowakumba watumizi wa barabara.
Kulingana na Kaimu meneja wa mji wa Malindi Jonson Mwabati Ukosefu wa alama hizo barabarani umekua chanzo cha watumizi wa barabra kukiuka sheria za trafiki mjini humo.
Akizungumza wakati wa kupokea alma hizo Mwabati, alisema kuwa ukosefu huo umechangi pakubwa ongezeko la ajali na uvunjaji wa sheria za barabarani
“ Tulikuwa na mkutano ya yeye hapo awali na alikuwa amekubali kuungana na sisi kama manispaa ili kuboresha mji wetu wa malindi katika idara ya trafiki ili kuhakikisha kwamba sheria zile za barabarani zinafuatwa vizuri na traffic flows ziko sawa” Alisema.
Haya yanajiri huku taasisi za mafunzo ya barabarani mjini malindi zikitoa wito wa kupokea mafunzo kuhusu sheria hizo na kuhamasisha kuhusu madhara ya ukiukaji wa sheria hizo