Kaunti ya Mombasa imetajwa kama moja ya kaunti zilizo na vijana wengi waliyokumbatia sanaa ili kujikimu kimaisha.
Haya ni kwa mujibu wa mkufunzi wa mambo ya sanaa kutoka shirika la utamaduni nchini (Kenya cultural center) Mbeki Mwalimu akithibitisha kuwa vijana wa kaunti ya Mombasa wamekumbatia sanaa kama ajira ikilinganishwa na vijana wa kaunti zengine nchini.
Katika kongamano la kutoa mafunzo kwa wasanii la County Theatre Fiesta linaloendelea katika jumba la sanaa la little theatre mjini Mombasa Mbeki alitoa wito kwa serikali kuu na zile za kaunti kuwawezesha vijana katika kutambua na kukuza talanta zao ili waweze kujitegemea maishani kama njia moja wapo ya kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira
“Kusema ukweli Mombasa Competition Iko juu, ule uigizaji tumepa huku Mombasa si kama kaunti zingine, so nimepata motisha hatuanzi kuwavuta kutoka kule mbali sana kwa sababu tunafanya capacity building kwahio kitu wanafaa kufanya ni kuwa na vigezo vya kujiutoa zaidi tu lakini Mombasa tuko juu” Alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa tamasha hilo Ngobia Benson aliwahimiza vijana kujitokeza na kijiunga na sanaa ikiwemo uzalishaji na uelekezaji filamu miongoni mwa sanaa nyigi nyinginezo.
Abdallah Saidi Pagawa ambaye ni msanii wa ngoma za kitamaduni za Gonda Asili alizitaka serikali za kanda ya Pwani kuwekeza zaidi katika sanaa sawa na kuwasaidia wasaii kutafuta masoko katika mataifa ya nje kama njia ya kuwakuza na kuimarisha sanaa zao.
“ ni vizuri zizidi kuwekeza na kutujali sisi kama vijana , kama wasanii na zaidi pia inaweza kuwa kaunti za pwani labda haziwezi kutulipa, kutusimamia kupitia sanaa lakini kule nje kama kaunti zinaweza labda waziri wa mambo ya nje iwe naweza sisi tupate ajira”. Aliongezea
Hata hivyo Mariam Swaleh miongoni mwa wasanii wanaopokea mafunzo kutokanana tamasha hilo aliwasihi vijana wa kike kujitokeza kwa wingi na kufaidi matunda ya ulimwengu wa sanaa akisema kuwa sanaa na talanta imepewa uzani sawa kwa wote wake kwa waume kote ulimwenguni.
“ kuna gender balance kuna wanawake 5 na wanaume5 kwa kila kikundi , lakini ningependa sana kuwapamotisha jamii ya kike tufanyeni hii kitu , hii industry haihitaji tu wanaume” Alisisitiza