Baadhi ya viongozi wa chama cha Wiper Kaunti ya Mombasa wamemshtumu vikali aliyekuwa seneta wa Mombasa ambae pia ni mbunge wa EALA Hassan Omar Sarai kutokana na matamshi yake dhidi ya kiongozi wa wiper Kalonzo Musyoka.
Mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Mombasa sheik Twaha Omar alimtaka Omara Sarai kumuomba msamaha Kalonzo kutokana na matamshi yake dhidi ya kinara huyo aliyoyataja kuwa dharau ya hali ya juu ikizingatiwa kwamba Sarai aliwahi kuhudumu kama katibu mkuu wa na kuchaguliwa kama seneta wa kwanza kaunti ya Mombasa kupitia tikiti ya chama hicho.
Kwa upande wake Twaha alishikilia kuwa iwapo sarai atadinda kuomba msamaha kiongozi huyo wa wiper, kama wananchama wa wiper kaunti ya Mombasa wataanza kampeni ya kuhakikisha kamwe Sarai hatachaguliwa tena kama gavana wa Mombasa.
“Twakuomba kwa haraka uombe msamaha yale ulioyasema nay ale uliomtamkia Kalonzo Musyoka bila hivyo tutafanya kampeni kubwa ya kuhakikisha vile alivyoema Kalonzo Musyoka hutawahi kuwa gavana. Ili kuitwa kiongozi amekuwa elected na Wiper senator wa kwanza Mombasa , yeye ni wa kushukuru na kumshukuru Kalonzo Musyoka , na hiyo ndivyo itakavyo kuwa hutawahi kuwa gavana Mombasa,” alisema Twaha.
Twaha vile vile alimtaka Sarai kuzingatia ngazi za uongozi na kutojilinganisha sawia na kiongozi huyo anayeshikilia wadhiwa kama kinara wa chama cha Wiper nchini Kenya.
“Kule kumkosea heshima kupewa nafasi kukaa naye kwenye kikao haimaanishi kwamba yeye ni saizi yake, Yule ni party leader. Leo twasikitishwa kumuona Hassan Sarai anamkosea hishima kiongozi kiongozi Kalonzo Musyoka mbele ya vyombo vya habari na mbele ya watu.” Aliongezea