Takriban Vijana milioni 1.9 wamenufaika kwa kupokea nafasi mbali mbali za kazi kutoka maeneo tofauti nchini Kenya .
Gracemerry Muchiri Afisa wa mawasiliano na mauzo kwenye programu ya Ajira Digital kutoka muungano wa kusimamia sekta za kibinafsi za Kenya maarufu KEPSA alithibitisha kuwa programu hii inayotoa jukwaa la nafasi za kazi kwenye mitandao ilisheheni ongezeko la vijana ambao wamekumbatia kazi hizi.
KEPSA vile vile ilichukua wajibu wa kuongea na makampuni na wafanyabiashara mbalimbali kwa niaba ya vijana hawa ili waweze kupata ajira mitandaoni jambo lililopelekea makampuni mengi kuajiri vijana wanaotumia mitandao ya kidigitali katika kazi zao kutoka sehemu mbalimbali.
“ Body ya private sector inaongelesha wamiliki wa biashara ili wawapatie kazi kijana si lazima awe katika ofisi zao, wanaweza wafanya kazi kama book keeping, data entry wanawezapata from ajira. Tuko hapa kuogelesha vijana wanaotutafuta riziki kuwa kuna nafasi mitandaoni na pia kuwajuza makampuni kuwa wanaweza kupata talanta ya haw vijana mitandaoni na pia kendeleza biashara zao” Alisema Muchiri
Kulingana na Muchiri swala la udukuzi na unyanyasaji mitandaoni limekuwa changamoto kuu na limewalazimu kuwapa vijana hawa mafunzo na ushauri ya jinsi ya kukabiliana na changamoto hizi ili wasikate tamaa.
“ issues za cyber bulling, vitu tunafanya tunafanya wakati wa mafuzo kukutrain kukabiliana na changamoto hizi na kukupatia akili za ujasiri amali, wewe ni mwana biashara hata ukipatikana na changamoto utajua jinsii ya kuzikabili” Alisema
Fauka ya hayo vituo vya uezeshaji vya kuwasaidia vijana ambao hawana uwezo wa kupata vifaa vitakavyo wawezesha kufikia mitandao vimefunguliwa sehemu mbalimbali nchini.
“ kulingana na ile takwimu ilifanyika ilipatikana kwamba zaidi ya vijana wakenya milioni 1.9 wanafanya kazi mitandaoni . Kuna wengi wameanza kuingilia suala hili na pia kampuni nyingi zimeanza kutafuta wafanyikazi wa dijitali” Aliongezea