Waandishi wa habari wanaopitia changamoto ya msongo wa mawazo na unyanyasaji wametakiwa kuwahusisha wanahabari wenza ili kuepuka visa vya kujitoa uhai.
Akizungumza na wanahabari hapa Mombasa, Mratibu wa Mipango kutoka Muungano wa Wanahabari Nchini, K.U.J, David Indeje alibaini kuwa waandishi wamekuwa wakipitia matatizo chungu nzima ambayo yamekosa kushughulikiwa na hivyo kupelekea baadhi yao kuchukua maamuzi magumu, ikiwemo hata kujitoa uhai.
Kulingana na Indeje baadhi ya waandishi wanaozongwa na msongo wa mawazo hunyamazia suala hilo na kuhatarisha maisha yao.
Indeje hata hivyo aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwalipa kwa wakati wafanyakazi wao ili kuepuka masuala ya waandishi kuzongwa na mawazo.
“Kama muungano tumeona idadi ya dhuluma kwa wanahabari wa kike inazidi kupanda na kwa sasa ni swala la dharua hivyo linahitaji litatuliwe kwa haraka”.Alisisitiza Indeje.
Wakati uo huo mratibu huyo alitoa lalama zake kwa kile anachodai ni ongezeko la waandishi wa kike kudhulumiwa wanapokuwa kazini, alisema kuwa suala la dhulma dhidi ya waandishi wa kike kuwa la dharura.
“Mwandishi wa habari unapoona kuna tatizo mahali zungumza na wenzako pasi kuogopa ili usaidike kwa uharaka hata kama linawakumba kama kikundi zungumzeni msinyamazie tu”.Alisema Indeje.
BY EDITORIAL DESK