Taasisi ya utafiti wa maswala ya baharini na samaki ya Kenya Marine and Fisheries Research Institute (KMFRI) imeanzisha mradi wa kuyasafisha maji ya chumvi kwa minajili ya wakaazi kunywa na kutumika kwa kilimo maarufu kama Sea Water Greenhouse Technology Mining from Saltworks.
Akizungumza na waandishi wa habari Kadzuhoni palipo na mradi huo ndani ya eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, afisa wa utafiti wa kisayansi kwenye taasisi hiyo Joseph Nyingi Kamau, alieleza kuwa mradi huo unatumia teknolojia ya upepo na jua na ukilenga kukabiliana na ukame pamoja na ukosefu wa chakula kwenye sehemu kame.
“Mradi huu unaojulikana kama Sea Water Greenhouse Technology and Lithium Mining from Saltworks unahitaji sehemu ambayo ikonajua kali na upepo mwingi ili uweze kufaulu. Hii Ndiyo maana hapa Magarini tulichagua sehemu hii ya Kadzuhoni kwasababu sehemu hii inajua kali na upepo ni mwingi,” alisema Kamau.
Kwa mjibu wa Kamau taasisi hi inalenga kupeleka mradi huo katika sehemu nyingine kame ikiwemo Bamba na Turkana ili kusaidia kupunguza changamoto za uhaba wa maji na chakula ambazo zimewakumba wakaazi wanaoishi maeneo hayo kwa muda mrefu.
“Mradi huu unaojulikana kama Sea Water Greenhouse Technology and Lithium Mining from Saltworks unahitaji sehemu ambayo ikonajua kali na upepo mwingi ili uweze kufaulu. Hii Ndiyo maana hapa Magarini tulichagua sehemu hii ya Kadzuhoni kwasababu sehemu hii inajua kali na upepo ni mwingi,” aliongezea.
William Kombe Fikiri ambaye ni mkazi wa eneo la Kadzuhoni, alipongeza taasisi hiyo kwa kuanzisha mradi huo kwenye sehemu hiyo akiongeza kuwa mradi huo utasaidia pakubwa wenyeji wa eneo hilo.
“Huu mradi ni mzuri kwa sababu kwanza kabisa ukikamilika jamii itanufaika kwa kupata kazi na wakipata kazi hapo ndipo pesa zitakapopatikana. Tutakuwa tumepata riziki yakuweza kujikimu kimaisha na kuzilea familia zetu,” alisema Fikiri.
Kulingana na Kamau, mradi huo unatumia mbinu rahisi sana ambayo inahusisha jua na upepo mkali na pia baada yakuyasafisha maji, lilerojo la chumvi ambalo hubakia linatumika kutoa madini aina ya Lithium ambayo yanatumika kutengeza beteri (battery).