Viongozi wa makanisa kutoka kaunti ya Kilifi wamekashifu vikali shinikizo la kubuniwa kwa sheria itakayoyalazimu makanisa kulipia kodi maalum kwa serikali za kaunti pale yanapotaka kufanya mikutano ya mahubiri na maombi.
Wakiongozwa na Askofu Thomas Kakala kutoka kanisa la JCC Malindi, viongozi hao waliikosoa hatua hiyo wakisema kwamba inahujumu uhuru wa kuabudu nchini.
Hata hivyo kwa pamoja viongozi hao walitoa pendekezo kwa serikali wakiitaka kutoruhusu utendwaji wa sheria hiyo wakisisistiza kwamba inakandamiza makanisa.
“Suala la utozaji usuru wa kamanisa, Kanisa si organization ambayo inafanya biashara kiasi cha kwamba hela wala tunawekeza hela. Mizigo ya kukata watu ushuru kila mahali mpaka imefikia mahali kuingia katika makanisa. Hatujawahi sikia duniani kote kwamba kanisa linakatwa ushuru ili kwamba nchi ikaweze kuendelea”
hii inajiri tu baada ya bunge la kaunti ya kisii kupitisha sheria itakayowatoza ada wahubiri kabla ya kuandaa kesha. Wahubiri kisii iwapo gavana Simba Arati Atatia saini sheria hio, basi watawajibika kulipa shs. 5,000 kila wiki kuandaa kesha, Shs. 2,000 akitozwa mhubiri atakayeingia mitaani kuenenza injili kwa wiki na Shs. 20,000 kwa wiki zikitozwa wahubiri watakaotumia magariya kubebea mizigo yenye vipaza sauti .