HabariNews

Kina Mama Hoyee! Jamii ya kike yataka Usawa na Kupewa kipaombele ndani Sekta ya Ubaharia

Kina mama katika sekta ya uchumi samawati kutoka ukanda wa pwani wameita idara husika kuwapatia kipau mbele kwenye sekta ya uchumi baharini kama njia moja wapo wa kuwainua ili kukidhi mahitaji yao.

Wakizungumza na vyombo vya habari wakati wa kupokea mafunzo kuhusu maswala ya ubaharia katika eneo la Kalro Mtwapa kaunti ya Kilifi yalioandaliwa na mashirika ya Go blue,blanket one,EU kwa ushirikiano serikali ya kaunti ya  Mombasa miongoni mwa mashirika mengine, kina mama hao waliitaja sekta ya ubaharia miongoni mwa zile zilizokumbwa na kasumba kwamba ni ya wanaume pekee swala ambalo walilipinga vikali na kutaka jinsia ya kike kuwezeshwa kikamilifu katika sekta hiyo.

Kulingana na Bakari Abdallah mhadhiri kutoka chuo cha kiufundi cha ukunda, imefika wakati kina mama kutambulika na hata kupewa nafasi za uongozi katika sekta hiyo ili kuwawezesha kikamilifu kando na mafunzo yanaondelea ambayo waliyataja kuwapa nuru kwenye sekta hio ya ubaharia.

Sisi tunataka wanawake wawezeshwe wapate mtaji ambao utawasaidia kujikimu katika biashara zao, pia wasaidiwe katika masuala ya ujuzi. Wale wanawake wawewanafundishwa masomo ili wawewanaweza kujifanyia wenyewe bila mtu kuwasimamia. Tunataka viongozi wa wanawake katika masuala ya blue economy.” Alisema

Amina bwanamkuu, mwenyekiti wa kikundi cha kina mama wanaojihusisha na maswala ya baharia na biashara ya samaki kutoka kaunti ya Lamu alisema kuwa kina mama ni tegemeo kuu katika jamii na nisharti maslahi yao yaangaliwe ipasavyo.

Hata kama ni ofisi pale ndani, kuna kufagia kuna kupanga maboksi na mambo mengi lakini utaona wanawake hawahusishwi wengi inaenda kwa wanaume. Tunaomba msaada kwa wingi kwa wanawake ili tusinyanyasike tuendelee wenyewe kama wanume wafanya wanawake twashindwa na nini wote ni sawa tu,” alisisitiza Amina.

Kwa upande wake mkurugenza katika wizara ya uvuvi na uchumi samawati kaunti ya Mombasa Aisha Mlingo, mafunzo hayo yatakuwa na manufaa makuu katika maisha ya kina mama kwani kama wadau tayari kuweka misingi dhabiti ya kuwawezesha kikamilifu.

Hii itamuezesha zaidi kupata ufahamu ili asibaki pale kwa kukaanga samaki pekeyake bali pia aendeleze ile biashara yake kwa njia tofauti tofauti, hii itatusaidia kuepuka ile changamoto ambayo tuko nayo pale ambayo kwamba tunapata wanawake wengi kabla upate yule samaki labda kuna njia ambayo lazima upitie, lakini tukiwa na miundo kwamba tumewafunza tumewawezesha na pia wamejielewa itakuwa bora zaidi kwao.” Aisha Alisema.

BY DAVID OTIENO