Wanaharakati wa kutetea na kulinda mazingira ya mnyama kasa eneo la maweni huko Mtwapa Kaunti ya Kilifi wanamtaka waziri wa madini, uchumi samawati na maswala ya ubaharia Salim Mvurya kutambua juhudi za vijana wanaolinga mazingira ya bahari.
Kulingana na Wanaharakati hao kutoka mradi wa Mtwapa-maweni turtle Conservation wanaofanya kazi ya kujitolea, juhudi zao za kumlinda kasa katika fuo za bahari katika kaunti hio zimetokomeza pakubwa wawindaji haramu baharini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mradi huo Micheal Mwaruwa, Ulinzi waliokuwawakiuweka nyakati za usiku kumesaidia kuweka mazingira salama ya mnyama kasa kutaga mayai na kukuza idadi yake baharini.
“ Tunaomba sana waziri Mvurya atukumbuke. Tangu tuanze kulinda kasa 2006 mpaka sasa hakua uuaji wa kasa labda kama ni kuuliwa ni ndani ya maji na sio katika fuo zetu tunazolinda. Hatuna vifaavya kumshika yule muhalifu kule ndani, hua tunamlinda kasa hapa ufuoni sana sana tunafanya usiku kisha asubuhi tunafanya day patrol,” Alisema
Kundi hilo hata hivyo lilijitolea kuendeleza hamasishwa katika jamii ya eneo hilo dhidi ya uchafuzi wa mazingira na uwindaji haramu wa mnyama huyo adimu.
“Jamii tumejaribu kuihamasisha ili wajue kwamba kasa ni kiumbe kilichohatarini na ni raslimali iliyo hai. Kitu ambacho tunaomba zaidi ni serikali yetu pia ije mashinani tuwe na vikao nao kuhusu fuo za bahari na ulinziwa kasa ama mazingira kwa jumla” Alisisitiza.
BY JOSEPH JIRRA