HabariNews

Serikali yaorodhesha Utumizi wa Mihadarati kuwa Tishio Kuu la Usalama wa Kitaifa sawia na Ugaidi

Serikali imeorodhesha utumizi wa Dawa za kulevya kama tishio kuu la usalama nchini baada ya ugaidi na visa vya uvamizi wa majambazi.

Waziri wa masuala ya kitaifa na Usalama wa Ndani Prof. Kithure Kindiki alitaja matumizi ya pombe haramu, dawa za kulevya kuwa miongoni mwa vitisho vikuu vya usalama wa taifa ikiwemo itakadi kali za kikabila, kidini na kisiasa.

Akiongea huko eneo bunge la Tetu Waziri Kindiki alisema kuwa Serikali inaimarisha zaidi uwezo wa Mamlaka ya Kitaifa ya kudhibiti mihadarati na pombe NACADA kuzuia usambazaji wa pombe haramu na dawa za kulevya dawa, ili kuipiga jeki katika vita dhidi ya utumizi wa mihadarati na pombe nchini.

Kwa upande wake NACADA ilianzisha mpango wa kufuatilia maendeleo ya watu waliopitia vituo hivyo baada ya kipindi chao cha kuratibiwa huku wakiwasaidia kuwapatia ujuzi wa shughuli za kuwaingizia mapato.

Mpango huu unalenga kuwaokoa vijana waliopotoshwa na wafanyabiashara wasio waaminifu na walanguzi kuingilia matumizi ya dawa ya kulevya.

BY MJOMBA RASHID