Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi ameunga mkono hatua ya serikali kuongeza ada ya stakabadhi muhimu licha ya pendekezo hilo kuzua mjadala miongoni mwa Wakenya.
Kulingana na Mwinyi nyongeza hizo za ada zitawafanya Wakenya kuwa waangalifu na kutunza vyeti hivyo badala ya kuvipoteza.
“Kulipa si viaya lakini ni kiwango gani hio ndio tatizo. Ni muhimu tuhimize watu wachunge hizi stakabadhi, kwaufupi ni lazima wananchi kidogo wachangamshwe lakini tunasema isiwe pesa nyingi sana, iwe pesa ambayo mtu anaweza kulipa” Alisema
Wakati uo huo Mwinyi alibaini kuwa kama mbunge wa mrengo Azimio atamkashifu na kumkosoa rais pale atakapowakosea Wakenya na vilevile kumsifia pale atakapowajibikia masuala yenye manufaa kwa wananchi.
Kiongozi huyo alimtaka rais Ruto kutembelea eneo bunge lake la Changamwe kuanzisha miradi ya maendeleo ikiwemo, ujenzi wa soko eneo hilo, kufufua mtambo wa usafishaji mafuta wa Kenya Petroleum Refinery, KPR miongoni mwa miradi mingine.
“ Kubadilika ni mpaka maombi makubwa sana lakini hatufai kuchukiwa kwa sababu group yetu ni O hapana, we are still Kenyas. Tuko na mahitaji hata sisi, tunataka tupatiwe kama ekari 20 hapa, Tunamtaka hapa kwa sababu kwa sasa yeye ndio rais wetu na sisi hata tukitoka nje tunasema rais wetu ni Ruto” Alisisitiza
Hata hivyo Kauli ya Mbunge huyo kuunga mkono hatua ya serikiali kuongeza ada za stakabadhi muhimu, ilikosolewa na kadhi mkuu nchini Sheikh Abdulhaliim Hussein Athman aliyesistiza haja ya serikali kuboresha huduma kwa wananchi na wala sio kuongeza gaharama ya maisha kwa Mkenya wa kawaida.
“ Kuko na muda fulani watu wanaoana nahakuna vyeti.tunashukuru kwamba pamoja na attorney general na sajili ya ndoa hilo tatizo limepotea saii, shida bado wananchi wanasema ada ni kubwa lakini attorney general amekataa kupunguza. Tunaomba serikali iangalie jambo la hivi vitabu hatakama serikali inavichapisha iwe ni ada ya kkuchapishia tu na sio biashara za cheti” Alisema Kadhi