HabariNews

Odinga Apinga matozo ya Serikali ya Vitambulisho na Pasipoti, aapa kusimama kidete!

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amekashifu vikali hatua ya serikali kupendekeza utozaji wa ada ya kujisajili kupata kitambulisho na kupata uraia kwa wageni.

Kulingana na Odinga ni haki ya kila Mkenya kupata kitambulisho bila malipo yoyote kwa ajili ya kupata huduma muhimu za serikali akisema hicho ndicho kigezo cha kutambulika kama mkenya halisi.

Akiongea katika kikao na viongozi wa kidini mtaani Westlands jijini Nairobi, Odinga aliikashifu serikali ya Kenya kwanza kwa kile alichokidai kama usaliti na unafiki kwa viongozi hao kutumia mwamvuli wa dini kuhadaa Wakenya ili kujinufaisha wenyewe swala alilosema halikuwa na ukweli kwa mwananchi wa kawaida.

Kitambulisho inatakikan kila mkenya apate bila ya kutoa chochote sababu wewe  ni Mkenya. Sasa wamesema ati ukiwa wewe Mkenya ukienda nje ukapate msichana huko ukaate mtoto huko, ili aje awe mkenya milioni moja, je hii ni ungwana? Mambo ya kitambulissho tutasemani llazima kila mkenya apewe kitambulisho.” Alisema

Kinara huyo wa mrengo wa Azimio aliweka wazi baadhi ya masuala makuu ambayo mrengo huo unashinikiza kutekelezwa katika kamati ya mazungumzo ya Kitaifa, akikariri kuwa hawatakubaliana na ripoti ya kamati hiyo iwapo haitagusia mapendekezo yao.

Masuala hayo ni pamoja na kutatuliwa tatizo la kupanda kwa gharama ya maisha, kuundwa upya kwa tume ya Uchaguzi IEBC, kukaguliwa kwa sava za IEBC miongoni mwa mengine.

Tunasema ile timu yetu ambayo iko pale mpaka watoke na matokeo vile Oparanya amesema, ambayo inaonyesha vile tutarekebisha mambo ya IEBC, pili waongee juu ya mambo ya gharama ya maisha, tatu mambo ya sava yafanyiwe ukaguzi ili ijulikane matokeo yaklikuwa namna gani. Tunataka gharama ya maisha , bei ya mafuta, bei ya unga , bei stima, bei ya sukari, nauli ya kusafiri ata kodi ya nyumba irudi chini,” alisisitiza

 Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Azimio wakiwemo aliyekuwa gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya, seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na mwakilishi wa kike wa Nairobi Esther Passaris.

BY NEWS DESK