HabariNews

Mbunge wa Kilifi Kunisi Akanusha Uwezekano wa Kushuka zaidi kwa Bei ya Mafuta

Swala la ongezeko la bei ya mafuta likiendelea kuwa kero kwa wananchi kwa kusababisha kupanda kwa gharama ya maisha, baadhi ya viongozi wametilia shaka kauli ya rais Dkt. William Ruto kwamba bei ya mafuta huenda ikashuka zaidi ifikapo mwezi Disemba.


Siku chache tu baada ya bei ya mafuta aina ya petrol kushuka bei kwa shilingi mbili, rais Dkt. William Ruto katika ziara yake kaunti ya Kirinyaga alitoa ahadi ya kushuka kwa bei ya mafuta zaidi ufikapo mwezi Disemba, hatua anayodai kuchangiwa na mikakati ya kibiashara inayoendelea kuwekwa kati ya taifa la Kenya na mataifa yanayozalisha mafuta.
….
Ni kutokana na kauli hii ambapo mbunge wa Kilifi kusini Ken Chonga alielezea wasi wasi wa kutekelezwa kwa ahadi hiyo, akidai kuwa mfumo uliotiwa sahihi wa kuhusisha serikali kwa serikali katika biashara hiyo una nyima fursa ya kuangaziwa upya bei ya mafuta mpaka mwezi Disemba mnamo mwaka 2024.
…….
Chonga aliinyoshea kidole cha lawama serikali kwa kuhusisha kampuni binafsi katika uagizaji mafuta humu nchini badala ya kutumia shirika la mafuta la kitaifa ama kuhusisha kampuni zilizo na uzoefu kwenye maswala ya mafuta huku akisistiza kuwa huenda kuna njama fiche katika biashara hiyo.
…..
Hayo yanajiri huku utata ukishuhudiwa kuhusu shehena ya mafuta yenye thamani ya shilingi bilioni 17 katika bandari ya Mombasa.

BY ERICKSON KADZEHA