HabariNewsUncategorized

Vuta ni vute za donge la Elnino, kaunti Zikisheheni Lawama

Jumla ya shilingi milioni 25 kati ya shilingi milioni 50 zilizotengwa na Idara ya Majanga Katika Kaunti ya Kilifi zimetumika katika kutoa misaada ya majanga mbali mbali kwa waathiriwa wa mafuriko.

Gavana wa Kaunti hiyo Gideon Mung’aro alisema kwamba Serikali yake haijapokea pesa zozote za kupeana misaada kutoka kwa Serikali ya Kitaifa bali inatumia pesa zilizotengwa wakati wa bajeti katika kupambana na majanga.

Mung’aro alidokeza kwamba Serikali ya Kaunti ya Kilifi inalenga kuongeza pesa hizo kutokana na bajeti ya ziada itakayowasilishwa Bungeni kabla ya mwisho wa Mwezi wa Disemba mwaka huu.

Sisi hatujapata kama ziko njiani watatwambia kwa sasa tunatumia pesa zetu amabazo tulitenga kwa maswala ya dharura ,tulikuwa tumeweka milioni 50 na hii wiki tutakuwa na baraza la dharura na mawaziri kuweka mipango zaidi.” Alisema Mung’aro

 

Haya yanajiri huku Naibu wa Rais Rigathi Gachagua akishikilia kwamba Kaunti zimepokea fedha hizo na hata kujikanganya zaidi kuhusu ni kiwango kipi kimesambazwa kwa magavana.

Kauli ya Gachagua Mnamo siku ya Jumanne akisema ni kima cha shilingi bilioni 10 zilizotolewa na November 22, alibadili kauli hio na kusema kwamba ni kima cha shilingi bilioni 2.4.

Serikali wiki jana ilitenga shilingi bilioni 2.4 na tutazidi kutoa fedha zaidi siku zinavyosonga.” Alisema Gachagua.

 

Haya yanajiri huku Baraza la magavana lilikanusha madai ya serikali kuu kuhusiana na pesa za elnino.

Kulingana na mwenyekiti wa baraza la Magavana ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Kirinyaga Ann Waiguru, serikali za kaunti hazijapokea mgao wowote wa pesa za kukabiliana na Elnino .

Aliongeza kuwa serikali za kaunti zinadai serikali kuu kima cha pesa billion 62.85 huku kaunti 27 zikidai serikali mgao wa fedha kima cha billioni 19.64.

Waiguru alidokeza kaunti 13 zinadai serikali kuu shillingi billioni 10.17 za mwezo wa oktoba.

Leo tunataka kuweka wazi kwamba Serikali za kaunti hazipokea fedha zozote kutoka kwa serikali kuu za kupambana mvua ya elnino badala yake kaunti ndizo zinadai serikali kuu kama ifuatavto takribani kaunti 13 zinadai 10.17 za mwezi wa oktoba huku kaunti 27 zikidai serikali mgao wa shilingi 19.64.” Alisema Waiguru.

Kauli ya Waiguru ilipigwa jeki na naibu gavana wa kaunti ya Wajir Abdulah Ahmed amesema taarifa kuhusiana na magavana kupokea mgao wa pesa hizo ni siasa na hakuna ukweli wowote.

Hakuna pesa yoyote ambayo kaunti imepokea kukabiliana na mvua ya elnino hadi kufikia sasa, magavana hawapaswi kutishwa hawapaswi kudharauliwa na sidhani iwapo kuna gavana yeyeote ambaye hawezi kufanya kusaidia watu wake. “

BY NEWS DESK