AfyaHabariNews

Serikali Yahimizwa kuweka Mikakati Kabambe Kuzima Joto la Saratani

Serikali za kaunti na serikali kuu zimehimizwa kuweka mikakati kwa vifaa vya kisasa  kushughuhulikia ugonjwa wa saratani.

Kulingana na mtalaamu wa ugonjwa huo mjini Mombasa Daktari Riaz Kasmani, asilimia 30 ya wagonjwa hukimbia matibabu punde tu wanapogunduliwa kuwa na ugonjwa huo huku wakihofia garama kubwa ya kutibia ugonjwa wa saratani.

Daktari Kasmani akiwaongoza wataalamu hao walizitaka serikali zote mbili kufanya hima ili kuwapunguzia mzigo wa garama ya matibabu wakenya wanaoendelea kupambana dhidi ya matibabu ya saratani wanayosema kuwa ghali mno.

tunafaa kuangazia jinsi tunaweza kuwekeza katika matibabu ya saratani, dawa za bei nafuu za saratani, jinsi tunaweza kupunguza matibabu ya saratani ikiwemo dawa za chemotherapy, city scans na vituo vya radiology sababu hio ndio inayohitajika  kwa uangalizi bora wa saratani” Alisema

Kenya inashikilia nafasi ya tatu ikiongoza kwa idadi ya juu ya vifo vinavyosababishwa na ugojwa wa saratani, hii ikiwa ni sawia na asilimia saba ya vifo nchini.

Ikumbukwe kuwa asilimia 60 ya walioathirika na ugonjwa huu ni vijana wenye umri wa miaka chini ya 70.

BY NEWS DESK