Maafisa wa usalama katika kaunti ndogo ya Tana Delta wameanzisha uchunguzi kuhusu mauaji ya Kijana mwenye umri wa miaka 15 ambaye mwili wake ulipatikana Jumanne 9, Januari 2024 katika eneo la Tulu-Hurara.
Inasemekana kuwa kijana huyo alikwenda malishoni kuchungua mifugo mapema Jumatatu 8, na hakurejea nyumbani hali iliyopelekea familia yake kupiga ripoti kwa kituo polisi.
Polisi pamoja na wananchi hatimaye waliupata mwili wa mwenda zake katika eneo hilo la Tulu baada ya juhudi za kumsaka huku ukiwa na majeraha ya kupigwa na kifaa butu mwilini.
Kulingana na kamishna wa kaunti hiyo Mohammed Noor tayari watu 2 wanazuiliwa na polisi kuhusiana na kisa hicho.
“ Tungeomba wananchi wa hapo tayari ACC wa huko na OCPD wameweza kuongea na hao waweke amani na wananchi wameomba wale waliohusika kwa hio mambo wakamatwe.So watupatie muda tufanye uchunguzi tuwezzze kukamata hasaa ile vijana walihuzika kwa ile mambo ambayo ilifanyika” Alisema Noor