Rais William Ruto amekariri kuwa kamwe hatokubali idara ya mahakama ihujumu miradi ya serikali ya Kenya Kwanza.
Rais aliendelea kukemea idara ya mahakama kwa kile alichokitaja kutumika na Upinzani kuhujumu miradi na ajenda za serikali yake.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Nyumba za Bei nafuu katika kaunti ya uasin Gishu Rais Alisema japo anaheshimu uhuru wa idara ya mahakama, hatochelea kuwakashifu wenye nia Mbaya katika mipango ya serikali.
Kiongozi wa taifa aliwanyooshea kidole cha lawama baadhi ya watu ambao anadai wamekuwa wakiwasilisha kesi mahakamani na kuhonga maafisa wa idara hiyo ili kukwamisha miradi ya serikali.
“ Nyinyi ambo muko kotini muko na kazi, wototo wenu wako na kazi, nyinyi hamuja wahi kulala njaa alafu unaenda kotini unanunua wakili unapeleka kotini unahongana eti hii kazi isimame hawa wototo wakenya wengine wakae bila ajira. Nataka iwaambie, hawa watu wako na Mungu na wako na mimi, tutapambana na nyinyi” Alisema
Kauli Ya Ruto iliungwa mkono na Naibu wake Rigathi Gachagua ambaye alishikilia kwa Mahakama Haiana Uwezo wa kumzuia wajibu aliopewa na Wananchi.
“ wewe umeajiriwa na hawa wananchi na wewe utachukua amri ya wananchi Mhesimiwa rais,” alisema Gachagua
Vile vile Rais Ruto alikosoa mrengo wa upinzani nchini akidai walikosa ajenda mwafaka ya kuendeleza taifa.
“ Na wale watu wa upinzani wawache kupiga makelele watuambie mpango wao tafauti nah ii yetu ni gani amabayo itapatiwa hawa vijana ajira” Aliongezea rais
Rais Ruto hata hivyo alishikilia kuwa serikali imejitolea kubuni nafasi zaidi za ajira kwa wakenya ili kuhakikisha inakwamua Uchumi wa taifa.
“ Katika gazeti laleo tumetangaza nafasi 2500 ya wauguzi wa Kenya watakaoenda nje kufanya kazi, kwa sababu tatizo kubwa la Kenya ni mambo ya ajira na ni jukumu la serikali wapate ajira kuhakikisha kuna mirani , mikakati ya jinsi ya kutoa nafasi za kazi kwa mamilioni ya wakenya wanaohitajia”