HabariNews

Viongozi wa Makanisa Wazinduka Usingizini na Kusuta Serikali.

Viongozi wa Kanisa kaunti ya Mombasa wamemtaka Rais William Ruto kuheshimu katiba na uhuru wa idara ya Mahakama.

Wakiongozwa na Mchungaji Peter Nene wa Kanisa la Milele PCEA, walisema hatua ya rais Ruto kuingilia idara hiyo inatoa taswira isiyofaa kwa uongozi wa taifa.

Nene aliongeza kuwa Kiongozi wa taifa anafaa kukumbuka kuwa aliapa kwa taifa kuwa atalinda taifa na vita alivyoanzisha dhidi ya mahakama huenda vikayumbisha udhabiti wa Taifa.

“Katika mikono mitatu ya serikali kila mkono unatakiwa kufanya kazi huru ndio nchi iweze kuendelea kwa sababu rais aliapa kulinda katiba,kuingiulia idara ya mahakama ni kinyume cha katiba.” Alisema Nene

Nene ameshinikiza viongozi wa dini kujitokeza na kuzungumzia vita hivyo licha ya kuwa kampeni nyingi wakati wa siasa zilifanywa katika sehemu za ibada.

”Tutaaibika tukisema serikali ni mbaya na ahadi hazijatimizwa tukikumbuka zilifanywa ndani ya makanisa yetu na hio ndio sababu imefanya kanisa liko kimnya,tukisema wafuasi watatuliza nyinyi mlituambia ndio njia nzuri mbona mwawapinga”.Alihoji Nene

Kiongozi huyo wa kanisa amekosoa hatua ya rais Ruto kutoa madai dhidi ya swala la ufisadi katika idara ya mahakama akisema rais anafaa kuwa na taarifa zilizodhibitishwa.

“Mtu wa kiwango kikubwa kama Kiongozi waTaifa hafai kutoa madai kama hayo,madai yanatolewa na mtu ambaye hana namna ya kufuatilia mambo,kutoa madai ni mambo ambayo hayajadhibitishwa,kiongozi akinena kitu inafaa kuthibitishwa.

By Medza Mdoe