HabariNews

Joto  Lazidi kwa rais Ruto, Mawakili Malindi wakiandaa maandamano

Chama cha mawakili tawi la Malindi kimepinga hatua ya Rais William Ruto kukutana na jaji mkuu Martha Koome kuwa na mazungumzo kuhusu shida ya ufisadi inayokumba idara ya mahakama.

Chama hicho kilishauri jaji mkuu na jaji wenzake   kufwata sheria na iwapo wataifuata sheria basi sheria hio aidha itawaunga mkono katika sekta hiyo.

Akizungumza na wanahabari mwenye kiti wao Conrad Atiang mjini Malindi aliwasihi majaji wote kuufwata sheria na watakaodharau idara hiyo watalaaniwa vikali wakiendelea kudhalilisha mahakama.

Na tunawasisitiza jaji mkuu na majaji kwa jumla wanaofanya chini ya mwamvuli wa mahakama kufuata sheria na wakifanya hivyo chama cha wanasheria kitawaunga mkono” Alisema

 Haya yanajiri siku chache tu baada ya wanasheria kauti ya mombasa kuandamana kuhusiana na madai yayo hayo.

Ikumbukwe kuwa mnamo siku ya Jumanne Kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga alitahadharisha Idara Mahakama dhidi ya kufanya mazungumzo na Serikali Kuu ikiongozwa na rais Ruto.

Odinga alisema mazungumzo baina ya idara hizo mbili yanatishia kuweka hatarini uhuru wa idara hiyo ya mahakama ambayo inapaswa kuendeleza shughuli zake huru.

BY NEWS DESK