Kinara wa Azimio amekosoa mkutano kati ya Rais William Ruto na Jaji Mkuu Martha Koome ulifanyika mapema leo katka ikulu ya Nairobi.
Raila alisema kuwa mkutano huo utaskuma muingilio wa serikali kwa shughuli za mahakama akitaja hatua ya jaji mkuu kukosa uwajibikaji.
Kulingana na Odinga iwapo kuna haja ya mazungumzo yangefanywa kwenye idara ya mahaka bali sio katika ikulu ya Rais.
“Ikulu ni jengo la serikali kuu. Hapo ndipo rais anapoishi. Iwapo kutakuwa na mazungumzo kuhusu masuala ya uongozi, yafanywe kwa njia isiyoegemea upande wowote, ” Raila alisema.
Hata hivyo Odinga amedokeza kuwa hatua hiyo imonyesha kuwa idara ya mahakama imetekwa na serikali akihimiza majaji kusimama kidete na kuilinda katiba.
“Mahakama imetekwa na serikali kuu na tumeona hili kabla. ilitokea chini ya utawala wa Bw. Moi, na tumejaribu kumuonya CJ wa sasa asishirikiane na serikali kuu” Aliongezea
Mkutano kati ya wawili umefanyika baada ya wao kutangaza kuwa wako tayari kufanya kikao kutatua tofauti kati ya serikali na idara ya mahakama.