HabariNews

Takribani asilimia 40 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa KCPE kote nchini wamesalia majumbani

Takribani asilimia 40 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa KCPE kote nchini wamesalia majumbani kutokana na hali ngumu ya Maisha.

Kulingana na msemaji wa wakfu wa Mradi wa Mtoto asome initiative Abdalla Gatana amesema hali hiyo imeweka wazi jinsi viongozi humu nchini wameshindwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuipa elimu kipaumbele akisema iwapo asilimia hiyo itasalia nyumbani huenda ikawa hatari zaidi kwa maendeleo ya taifa.

Aidha Gatana amesema ipo haja ya viongozi mbali mbali kujitokeza ili kufadhili wanafunzi na kuhakikisha kuna asilimia mia kwa wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza.

“Viongozi kwa sehemu moja ama nyingine wameshindwa kutekeleza majukumu yao kama kulikuwa na kitu ambacho kinastahili kupewa kipaumbele ni elimu,hii asilimia 40 nauhakika itakapokosa elimu itakuwa imeharibu maendeleo katika jamii,lazima washikadau wazazi walimu na jamii kwa jumla tuweze kushirikiana.” Alisema Gatana.

Kwa upande wake Hamisi Dzilla mratibu wa mradi huo amesema kuna haja ya hamasa zaidi kutolewa kwa vijana kujitokeza kusomea kozi za mda mfupi akisema licha ya serikali kutoa ufadhili kwa vijana kusomea taaluma hizo vijana wengi bado hawajafahamishwa kiuhusu mpango huo inavyostahili.

“Kuna ule mfumo mafunzo ya vyuo vya kuifundi ambao umegawanya masomo ya vyuo vikuu mara mbili,ya kwanza nyanjani na ya pili darasani na serikali inatoa ufadhili lakini shida ni watoto wetu bado hawaelewi na kuna haja ya hamasa zaidi kutolewa.” Alisema Dzilla

By Medza Mdoe