HabariNews

Msako wa Wanafunzi ambao Hawajajiunga na Kidato cha 1 Waendelezwa Malindi

Msako mkali umeanzishwa na maafisa wa serikali huko Malindi kuwasaka wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao kujiunga na shule za upili.

Ikiwa njia mojawapo ya kutekeleza agizo la serikali la kuhakikisha kuwa na asilimia 100 ya mpito wa wanafunzi kujiunga na shule za upili hasa baada ya kumalizika kwa KCPE katika mfumo wa 8-4-4, msako huo unajiri huku ikibainika kuwa idadi kubwa ya wananfunzi haijajiunga na shule za upili eneo hilo.

Kulingana na Chifu wa Tezo-Mtondia, Henry Kingi asilimia 50 ya watoto waliotarajiwa kujiunga na shule za upili hawajafanya hivyo, akiwalaumu wazazi kwa kutowajibika kwao kumepelekea kushuhudiwa hali hiyo.

Hata hivyo Chifu huyo amewataka wazazi kushirikiana ili kufanikisha agizo la serikali linalolenga kuimarisha viwango vya elimu eneo hilo ambavyo vimedorora kwa muda mrefu.

BY ERICKSON KADZEHA