Wakulima eneo la Pwani wamehimizwa kutumia mbolea ya kiasili badala ya kutumia mbolea yenye kemikali kama njia ya kuboresha uzalishaji wa chakula na kupambana na baa la njaa.
Katika mahojiano ya kipekee na meza yetu ya habari Alhamisi 15 Florence Hela kutoka shirika la utengenezaji mbolea asili la Afya Duara Organic Enterprise alisema mbolea inayotengenezwa na kemikali hupunguza nguvu ya mchanga hivyo kupunguza zao la mimea.
Aidha Florence alidokeza kuwa itakuwa bora hata zaidi iwapo wakulima watakumbatia utumizi wa mbolea asili inayotengenezwa kutokana na takataka zinazooza kama vile mabaki ya chakula na uchafu wa sokoni.
“Tunawahimiza wakulima wajaribu kutumia mbolea asili kwa sababu inatengeneza mchanga kumbuka ile mbolea yenye kemikali inaboresha mmea sasa yule mwenye alipanda mwaka jana alipata mazoa akipanda mwaka huu atakuw ana mazao kidogo kwa sababu huo mchanga ushaharibika kutokana na kemikali zilizoko kwenye hio mbolea.” Alisema Florence
Wakati huo huo Florenece alihimiza wakazi eneo hilo kukumbatia mfumo wa utenganishaji taka kama njia moja ya kurahishisha kazi ya vijana wenye ubunifu wa kutenegneza vitu kutokana na taka hizo pamoja na kuimarisha usafi jijini humu.
“Tunachukua huo uchafu tunatengeneza mbolea na ule uchafu mwingine kama plastiki tunauzia kampuni za kutengeneza vitu vingine,taka ni mali na inaweza kumpa mtu pesa na pia tunaweza kuimarisha usafi wa mazingira yetu.” Alisema Florence.
BY MEDZA MDOE