HabariNews

Mwanamke mmoja anayedai Kuzaa na Marehemu Kiptum afika Kortini kuzuia mazishi Yafanyike

Hii baada ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 22 kudai kuwa alizaa mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba na marehemu.

Katika ombi lake mbele ya Jaji Robert Wananda, Edna Awuor Otieno, aliitaka mahakama kusitisha mazishi hadi pale atakapotambuliwa pamoja na mwanawe kama watakaonufaika na mali ya marehemu.

Kupitia cheti cha dharura, Edna aliiomba korti kuzuia Mwili wa marehemu kutoka katika makafani ya hospitali ya Eldoret hadi pale pande zote mbili zitakaposikizwa.

Kadhalika, Edna, kupitia kwa wakili wake Joseph Ayaro, ameiomba mahakama kutoa amri ya kuchukua sampuli za DNA na kupelekwa kwenye Taasisi ya Utafiti wa Matibabu KEMRI ili kuthibitisha ukweli wa madai yake.

Mwili wa mwanariadha huyo leo Alhamisi umeondolewa kutoka makafani ya hospitali ya rufaa Moi Eldoret.

Mwili huo umezungushwa katika mitaa mbalimbali ya mji wa Eldoret kaunti ya Uasin Gishu kama njia moja wapo ya kumpa heshima mwanariadha huyo.

Baadaye mwili huo ulifikishwa uwanja wa michezo wa Iten kaunti ya Elgeyo Marakwet ambako wananchi wamepata fursa ya kuutazama na kisha.

Ibada ya mazishi ya Ijumaa itahudhuriwa na rais William Ruto, naibu wake Rigathi Gachagua, na viongozi wengine wa ndani na nje ya nchi pamoja na wanariadha mbalimbali duniani.

Mwili wa Kiptum utazikwa nyumbani kwake kaunti ya Uasin Gishu hapo kesho Ijumaa.

BY CYNTHIA OCHIENG