HabariNewsSiasa

WAFUASI WA ODINGA KUSALIA MAYATIMA WA SIASA

Hatua ya Bwana Odinga kutangaza rasmi azima yake ya kuwania wadhifa wa Mwenyekiti wa AU, sasa inazidi kuibua maswali chungu nzima miongoni mwa wafuasi wake ambao wanataka kujua Mustakabali wa ki siasa wa kigogo huyo wa siasa nchini. Kuchaguliwa kwa Odinga kama mwenyekiti wa Muungano huo,kanuni za AU zitamwekea vizingiti na vikwazo kadhaa hali ambayo inawatia tumbo joto waandani wake wa karibu na pia wafuasi wake kote nchini.

Huku Odinga tayari akiwa ameanza safari ya kutafuta uungwaji mkono katika mataifa 55 ya wanawachama wa AU. Ni kanuni za Muungano huo ambazo zinazoiweka hatima na mustakabali wa siasa wa kigogo huyo wa upinzani nchini Mashakani.Lakini kwa nini AU, mbona sasa?Je, kuteuliwa kwake kutamweka Bwana Odinga katika mazingira ya aina gani?

Hatua hiyo ya Bwana Odinga iliwapata wakenya ghafla na sasa imewaacha wengi wa wafuasi wake na maswali chungu nzima kuhusiana na mustakabali wa hatua aliyochukua na sasa wengi wamesalia roho mkononi wakihofia kusalia solomba siasani.

Iwapo Odinga ataidhinishwa kama mwenyekiti wa Muungano wa AU, basi atatakiwa kutekeleza kanuni za Fedha za Muungano huo. Aidha litakuwa jukumu lake kuwa mwenyekiti wa mikutano na mijadala yote ya Tume na Baraza kuu la AU. Isitoshe, Waziri huyo mkuu wa zamani nchini atatakiwa kukuza malengo ya Umoja wa Afrika mbali na kuwasilisha taarifa kwa Bunge na Halmashauri kuu ya Muungano huo.

Pia, Ofisi yake Odinga itakuwa na jukumu la kuhifadhi miktaba yote ya AU huku vyombo vya kisheria vya muungano huo vikisalia mikononi mwake Bwana Odinga.

Maisha na tamaduni za kigogo huyo wa siasa nchini huenda pia yakabadirika pakubwa kwani Kanuni za AU, hazitamhurusu Bwana Odinga kuendelea kushikilia nafasi za kisiasa nchini. Kadhalika iwapo iwapo Waziri huyo mkuu wa zamani ataidhinishwa, sasa atatakiwa kuwa na busara na kujitenga na hatua za kuunga mkono mrengo wa siasa au hata kuendesha mikutano ya umma kwa nia ya kumpigia kampeini za siasa mgombea fulani.

Odinga kadhalika hataruhuhusiwa kuwa mgombea wa wadhifa mwingine katika ofisi nyingine anayoimezea mate au hata kukubali kuteuliwa katika ofisi ya nyingine ya umma nchini. Pia Bwana Odinga, atazuiliwa na kanuni hizo kushiriki shughuli zozote za siasa nchini.

Hata hivyo, kanuni za AU zitamruhusu Odinga kusalia na haki ya kupiga kura nchini Kenya.

Wafuasi wa Odinga, sasa wahofya Kanuni hizi huenda zikamwondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais mwaka wa 2027.

Wanachama wa AU wanatarajiwa kutoa uamuzi wao mwaka ujao huku atakayechaguliwa akiwa na kipindi cha miaka minne kuudumu kama mwenyekiti wa Muungano huo.

Hivyo iwapo ni Odinga atakayemrithi mwenyekiti wa sasa Musa Faki, basi atakamilisha hatamu ya ya kuudumu katika ofisi hiyo mwaka wa 2028, hali ambayo huenda ikawafanya wafuasi wa Odinga kukosa jina lake debeni mwaka wa 2027

BY ISAIAH MUTHENGI