Huku zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya taifa la Kenya kujiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya wanawake duniani,, Viongozi wanawake humu nchini wamehimizwa kushirikiana kuhakikisha wanafanya maendeleo ya wanawake.
Akizungumza eneo bunge la Kaloleni mnamo Jumatano katika maandalizi ya maadhimisho ya Siku hiyo inayoadhimishwa kote duniani kila tarehe 8 mwezi Machi, Mwanaharakati wa maswala ya siasa Chitsao Kahindi amewarai viongozi wanawake walio mamlakani kuhakikisha wanawekeza zaidi kwa wanawake ili kukabilaiana na changamoto ambazo wanawake wanapitia.
Aidha Kahindi alipongeza juhudi za naibu wa gavana wa kaunti hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika maswala ya maendeleo na ushirikianao eneo hilo.
“Ni jukumu la viongozi kuhakikisha hawa kina mama hawaombi ombi ,nyinyi viongozi kina mama naomba mkae na naibu gavana nimeona ni mtu wa kupenda maendeleo. “ Alisema Kahindi.
Kwa upande wao Raphael Garama na Frida Mohammed ambao pia ni waharakati wa siasa eneo hilo waliwataka kina mama eneo kuwajibikia majukumu yao na kuwachagua viongozi walio na maadili ya uongozi yatakayostawisha maendeleo ya wanawake eneo hilo.
“Kitu mimi naomba kina mama muwajibike ,viongozi wetu twaomba mtushike mkono lisiwe hili bali kuwe na maendeleo ,hiki kiti tujue twampa nani na ni nani atakayetufaa kama kina mama maana kina faida ndani yetu kina mama.” Walisema
Naye Seneta mteule wa zamani kaunti ya Kilifi Christine Zawadi amemtaka gavana wa kaunti hiyo Gideon Munga’ro kuwashika mkono kina mama kwa kuwapa zabuni za Serikali zitakazowafaidi kina mama huku akimtaka kuwa makini na wale wanaowasilisha vyeti ghushi ili kupata zabunoi za serikali.
“Washike wamama wa kuhesabu ili nao pia wafaidika na zile zabuni za serikali halafu kuna watu wametengeneza vyeti ghushi kwamba wao wametimiza zile sheria za mama wala sio kina mama.” Alisema Zawadi.
Siku ya Kimataifa ya Wanawake ilibuka mara ya kwanza kutokana na harakati za wafanyakazi mwanzoni mwa karne ya 20 huko Marekani Kaskazini na kote Ulaya na ilitambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1977.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku hii mwaka huu Ni: Wekeza kwa Wanawake, kuongeza kasi ya maendeleo.
BY MEDZA MDOE