AfyaHabariNews

AFUENI KWA WAKAAZI WA MOMBASA, AFYA YA MSINGI IKITUA MASHINANI.

Katika juhudi za kuimarisha sekta ya afya mashinani serikali ya kaunti ya Mombasa imefanya kikao na washikadau mbali mbali katika juhudi za kubuni mifumo itakayounganisha huduma za kimsingi pamoja na vikundi vinavyofanya kazi kukinga magonjwa mashinani.

Akizungumza wakati wa kikao hicho mnamo Ijumma,15 Afisa wa Afya kutoka eneo bunge la Changamwe Micah Nyamosi alisema jamii inahaki ya kupata huduma za kimsingi za afya karibu nao na kwa bei ile wanayoweza kumudu huku akihimiza jamii kuchukua jukumu la kuhakikisha wanalinda afya zao kikamilifu.

Aidha Nyamosi aliongeza kuwa wanashirikiana na serikali kuu pamoja na wahudumu wa afya nyanjani kuhakikisha wanatimiza agenda ya serikali ya huduma afya kwa wote(UHC) kwa vision 2030.

“Leo tumeketi na washikadau ili tuangalie vile tutangeneza mifumo ya afya ya kimsingi ili kufanikisha maneno ya afya mashinani,kila ,mmoja anatakikataka kupata huduma za afya karibu naye na yenye malipo ambayo anaweza na ni kitu ambayo wao wenyewe watashirikishwa na wakuwe na maoni yao kuhusiana na huduma wanazopewa.” Alisema Nyamosi

Wakati huo huo Nyamosi aliwarai wanajamii kutembelea vituo vya afya wanapohisi mauvimu ama dalili za ugonjwa ili kutibiwa na madkari waliohitimu badala ya kununua dawa kwenye maduka ya rejareja ya kuuza dawa mitaani akisema hatua hiyo inahatarisha afya za watu wengi.

“Wanajamii wacha tuchukua majukumu ya afya zetu tuiweke kipaumbele ya kwamba ukiumwa na kichwa ama viungo usiende kununua dawa nenda katika kituo cha afya pimwa na mhudumu aliyehitimu ujue unaugua nini kabla hujameza dawa yoyote ,dawa zingine zinamadhara ukimeza kama hujapimwa ama umemeza hii dawa ukapunguza makali lakini kumbe ugonjwa uko ndani.” Alisema Nyamosi.

Ni kikao kilichohudhuriwa na viongozi mbali mbali ikiwemo Kamshina wa Chagamwe,Kiongozi wa watu walio na uwezo tofauti ,viongozi wa kidini kutoka baraza la waislamu na maimu nchini SUPKEM ,mashiririka ya kijamii na wengineo.

BY MEDZA MDOE.