Kwa mara nyingine tena Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amewataka madaktari kukubali kurejelea mazungumzo na serikali.
Nakhumich amewasihi madaktari kulegeza msimamo wao na kusitisha mgomo misha kushiriki mazungumzo akisisitiza kuwa serikali inafanya kila liwezalo kuhakikisha suluhu inapatikana.
“Tunafanya kile tuwezalo kusuluhisha mgogoro uliopo lakini kile ambacho hatutaki kufanya kama serikali ni kuweka bendeji kwenye kidonda bila kukitibu…” alisema.
Naye Katibu wa Afya Mary Muthoni Kariuki amewasihi madaktari wanaoendeleza mgomo kusitisha mgomo wao na kukubali kutoa nafasi ya mazungumzo kati yao na serikali.
Muthoni amesema wasiwasi wao madaktari unaweza kushughulikiwa kwa muda kando na serikali kusikiliza lalama zao akisisitiza kuwa masuala yote 19 yanayoshinikizwa na madaktari hayawezi kutekelezwa kwa siku moja bali kwa wakati mwafaka kupitia maafikiano.
Haya yanajiri huku madaktari wakiendelea kushikilia matakwa yao na kwamba hawatarejea kazini hadi yatakapotekekezwa.
Mgomo huo umeingia siku ya 34 sasa.
BY MJOMBA RASHID