HabariLifestyleNews

Serikali kuhitajia zaidi ya Bilioni 25 Kukarabati Barabara na Miundomsingi iliyoharibiwa na Mafuriko

Zaidi ya shilingi bilioni 25 zinahitajika na Serikali kuu ili kurekebisha barabara zote zilizosombwa na kuharibiwa na mafuriko nchini.

Kulingana Wizara ya Uchukuzi, Serikali inakadiria kuhitajia kima cha fedha kuanzia shilingi bilioni 25 hadi 30 ili kukarabati na kurejesha miundomsingi ya barabara katika hali yake ya awali.

Akizungumza mnamo Jumatano Mei 15 alipozuru kaunti ya Lamu kutathmini athari ya mafuriko kaunti hiyo, Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen alibaini kuwa mafuriko yamesababisha hasara kubwa ambayo itahitajia kima kikubwa cha fedha kukarabati miundomsingi iliyoharaibiwa.

Tumeathirika sana kama taifa na kama wizara ya uchukuzi na barabara, tumepoteza miundomsingi hasa barabara na madaraja, hadi sasa tumefanya utafiti na ingawa tutoa makadirio halisi.

Fedha tunazohitaji ni nyingi sana kurudisha miundomsingi ifike mahali ilikuwa na tunakadiria kati ya shilingi bilioni 25 mpaka 30.” Alisema Murkomen.

Murkomen alisema tatizo la barabara ya Lamu hasa eneo la Gamba limeendelea kuwa changamoto kwa wafanyabiashara na mataifa yanayoegemea uchukuzi na huduma za bandari ya Lamu hasa baada ya uchukuzi wa shehena kukwama bandarini kutokana na kuharibika kwa barabara eneo hilo.

Bado tuko na shida hapa Gamba na shida hiyo imetupa hasara kubwa sana ya kibiashara. Tulikuja kufanyia biashara bandari ya Lamu, LAPSET na wafanyabiashara wetu wakakubali kutumia poti hii ya Lamu kufanya biashara hasa mambo ya mbolea. Wameleta tani 60,000 ya mbolea na wakati imefika hata tulikuja hapa na mawaziri kutoka nchini ya Ethiopia kupokea mbolea hii sasa tunapata hii shida ya mafuriko.” Alisema.

Waziri huyo wa Uchukuzi hata hivyo alitoa hakikisho kwa wafanyabiashara wa taifa la Ethiopia kuwa serikali inafanya jitihada zote kuhakiisha mizigo hiyo inafikishwa nchini mwao.

…Kwa hivyo tumekuja hapa kuwakikishia wanabiashara kutoka Ethiopia na nchi ya Ethiopia kuwa tunafanya kila liwezekanalo kuhakikisha mizigo hiyo imeweza kufikishwa kwa sababu wakati huu huko Ethiopia ni wakati wa kupanda huko na wanahitaji mbolea yao wafanye ile kazi wanataka kuifanya.” Alisema Murkomen.

BY MJOMBA RASHID