HabariNews

Wahisani wajitokeza Kuwapa Wakazi wa Mombasa Afueni ya Taabu ya Matibabu

Hali ngumu za maisha ikiwemo uchumi umepelekea wananchi kutafuta mbinu mbadala za matibabu haswa wanapopatwa na matatizo ya kiafya.

Hata hivyo, zaidi ya watu 200 walipata fueni mnamo umamosi Mei 25 baada ya kujitokeza kupata matibabu ya bure katika zahanati ya kijamii chini ya ufadhili wa muungano wa wafanyabiashara kutoka jamii ya Pakistan, Star Of Hope.

Kwa mujibu wa daktari bingwa wa zahanati hiyo Dr. Haroon Saeed ni kuwa zahanati hiyo hupokea zaidi ya watu 100 kila siku na kupata matibabu kadhaa yakiwemo huduma za matibabu ya meno, macho, vipomo vya maabara na huduma kwa wagonjwa wa kisukari huku wakipania kufungua hospitali kubwa zaidi itakayoweza kuhumia wagonjwa wengi na kupata hudumu bora aidi kwa malipo ya shilingi mia pekee.

Dr. Haroon Saeed, Star Of Hope

Kufuatia hatua hii ya utoaji wa huduma bure viongozi na makundi mengine ya kijamii wametakiwa kuunga mkono hatua hizi ili kusaidia jamii ambao wengi hawana uwezo wa kulipia matibabu hayo katika hospitali nyengine.

Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Hassan Omar Sarai alieleza kuwa ipo haja kila mwenye uwezo kuunga mkono hatua sawia na hizo huku akitoa msaada wa shilingi elfu hamsini kusaidia katika shughuli za matibabu.

Hon. Hassan Omar Sarai

Muungano huo wa star of hope aidha umeeleza kuwa hivi karibuni wataongeza huduma zao za bure kwa wananchi kwa kufungua hospitali ya matatizo ya macho jambo ambalo daktari Haroon Saeed ameeleza kuwa litapunguzia wananchi gharama za kusafiri nje ya nchi kupata huduma hizo ikiwemo kufanyiwa upasuaji.

BY SOPHIA ABDHI