Uncategorized

Afueni kwa watumizi, wakulima na wafanyabiashara wa mugukaa serikali ikipinga marufuku ya bidhaa hiyo Ukanda wa pwani

Wakulima na wafanyabiashara wa muguka huenda wakapata afueni baada ya rais William Ruto kutaja marufuku yaliowekwa dhidi ya bidhaa hiyo kwenye kaunti za Mombasa, Kilifi na Taita Taveta kuwa sio halali.

Kwenye kikao kilichowaleta pamoja viongozi wa Embu, waziri wa kilimo na rais mnamo Mei 27 wiki hii, rais na Linturi walisema marufuku hiyo sio halali kwani bidhaa hiyo inalindwa kulingana na sheria ya kenya.

Kulingana na viongozi hao, mugukaa na miraa ni bidhaa zinazotambuliwa na sheria za kitaifa na hivyo sheria yoyote inayoenda kinyume na sheria ya kitaifa ni haramu na haifai.

Kupitia kwa taarifa kutoka Ikulu, waziri wa kilimo alimwambia rais kuwa sheria ya mwaka 2023 ya kudhibiti mazao ilipitishwa na bunge la kitaifa na lile seneti pamoja na makubalinao ya baraza la magavana.

Ili kushgughulikia sintofahamu iliyopo, rais aliagiza wizara ya kilimo na wadau wengine kuwahusisha wahusika wote kujadili suala hilo na kupata suluhu mwafaka.

“Ili kushughulikia matakwa ya pande zote na wadau, wizara ya kilimo na mifugo imeagizwa kufanya kiako cha majadiliano kuangazia lalama zilizoibuliwa na kukubaliana kuhusu utekelezwaji wa sheria ya mira/muguka mwaka 2023,” alisema rais William Ruto kwenye taarifa.

Hata hivyo rais alitangaza kwamba serikali itatenga shilingi milioni 500 kuwekezwa katia harakati za kuongza ubora wa bidhaa hizo kwenye bajeti yake yam waka 2024/2025.

Rais William Ruto baada ya kikao na viongozi wa Embu kujadili marufu ya Muguka

Haya yalijiri baada ya siku ya Alhamisi wiki jana Gavana wa mombasa Abdulswamad Sharif Nassir kutangaza marufuku ya bidhaa hiyo.

Siku moja baadaye Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro akafuata mkondo sawia na huo  na kutangaza marufuku kabla ya gavana wa Taita Taveta kumaliza orodha ya kaunti zilizotangaza marufuku hiyo.

Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya Kwale alipowahutubia waandishi wa habari mnamo Jumamnne ya Mei 28 mwaka huu alisema kwamba hatapiga marufuku bidhaa hiyo.

“Kama leadership ya klaunti tuanaoungana na wengine kupiga vita utumizi wa muguka. Of course hatutoweka ban kwa utumizi wa muguka kwa sababu ya kisheria, lakini pia tunafuatilia zile njia za kisheria ili kuhakikisha utumizi wa muguka unakuwa regulate,”alisema Achani.

BY MAHMOOD MWANDUKA