HabariNews

Gavana wa kwale akaidi wito wa wenzake na Kukataa Kupiga Marufuku Muguka

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amesema serikali yake haitapiga marufuku dhidi ya biashara na utumizi wa mugukaa.

Kwenye kikao na waandishi wa habari mnamo Mei 28 Achani alieleza kwamba hatua ya kutofuata mkondo wa kupiga marufuku kama magavana wengine unatokana na sheria zilizopo za kudhibiti bidhaa hiyo.

Aliongeza kuwa wanafuatilia njia zote mwafaka za kisheria kuhakikisha utumizi wa muguka unadhibitiwa katika njia inayofaa.

“Kama leadership ya kaunti tuanaoungana na wengine kupiga vita utumizi wa muguka. Offcourse, hatutoweka ban kwa utumizi wa muguka kwa sababu ya kisheria, lakini pia tunafuatilia zile njia za kisheria ili kuhakikisha utumizi wa muguka unakuwa regulate,” alisema Achani.

Mnamo Mei 23 gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir alipiga marufuku biashara na utumizi wa muguka.

Kwengineko serikali za Kilifi na Taita Taveta pia zilifuata mkondo sawia na kupiga marufuku dhidi ya bidhaa hiyo.

Hata hivyo, kulingana na rais William Ruto na Waziri wa kilimo Mithika linturi mugukaa unatambuliwa kisheria baada sheria ya kudhibiti mazao ya 2023 kupitishwa na bunge la kitaifa, bunge la seneti na makubaliano ya baraza la Magavana.

Katika kikao hicho kilichowajumuisha viongozi kutoka kaunti ya Embu rais mnamo siku ya Jumatatu Mei 27, serikali iliahidi kuwekeza shillingi milioni 500 kuongeza ubora wa bidhaa za mugukaa humu nchini.

BY EDITORIAL DESK